TIMU za
Stand United na Mwadui FC za Shinyanga zinatarajiwa kufungua dimba la
mashindano maalum yanayozikutanisha timu za ligi kuu zilizopo kanda ya ziwa
Victoria siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga.
Mashindano
hayo yameandaliwa na Chama cha Soka Shinyanga (SHIREFA), kwa kushirikiana na
kampuni ya Cleverland Res ya Mwanza na yatazikutanisha timu zote zilizopo ligi
kuu za ukanda huo
Akizungumza
jijini Mratibu wa mashindano hayo, Kabole Kahungwa alisema michuano hiyo
itakuwa ikichezwa kila siku kuanzia Agosti 8-12 kwa mtindo wa ligi ili kuzipa
maandalizi timu za Kanda ya Ziwa kabla ya Ligi Kuu.
“Kama unavyoona timu za Kanda ya Ziwa zimefanya usajili mzuri kuelekea Ligi Kuu, kwa hivyo na sisi tumeona tuziandalie mashindano baina yao ili kujiweka fiti, kabla ya ligi kuu kuanza”, amesema Kahungwa.
“Kama unavyoona timu za Kanda ya Ziwa zimefanya usajili mzuri kuelekea Ligi Kuu, kwa hivyo na sisi tumeona tuziandalie mashindano baina yao ili kujiweka fiti, kabla ya ligi kuu kuanza”, amesema Kahungwa.
Pia
alizitaja timu hizo kuwa ni Stand United, Mwadui FC zote za Shinyanga, Toto
African ya Mwanza na Kagera Sugar ya Kagera.
Ligi Kuu
inatarajiwa kuanza Septemba 22, huku kanda ya Ziwa msimu huu ikiwa na timu
nne, baada ya Toto African na Mwadui FC kupanda msimu huu na kuungana na Kagera
Sugar na Stand United.
Ratiba ya
mashindano hayo ni kama ifuatavyo, Agosti 8 ni Stand United Vs Mwadui FC,
Agosti 9 ni Toto African Vs Kagera Sugar, Agosti 10 ni Mwadui FC Vs Toto
Africans, Agosti 11 ni Kagera Sugar Vs Stand United, Agosti 12 ni Stand United
Vs Toto African na Agosti 13 ni Mwadui FC Vs Kagera Sugar
No comments:
Post a Comment