ALIYEWAHI kuwa golikipa wa vilabu vya Simba
na Yanga, Juma Kaseja na mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Jerryson Tegete
huenda wakajiunga na klabu ya Mwadui FC kwa msimu huu.
Hayo yamesemwa na Kocha Mkuu wa klabu hiyo
Jamhuri Kihwelo na kusema kama mambo yataenda kama yalivyopangwa atawasajili
ili waweze kuonyesha uwezo wao mkubwa.
“Mimi
nimeshasajili wachezaji 26 wanatosha, lakini wachezaji pekee ambao kama mipango
yangu itaenda sawasawa basi kuna mpango wa kuwaongeza ni Juma Kaseja na Jerry
Tegete kwasababu ni wachezaji ambao nimezungumza nao na wameniambia wanataka
kucheza na hawakuweka mbele kipato, na wamenivutia, tunataka tuwatumie kucheza
ili tupate mafanikio kwenye ligi”.
Julio pia aliweka wazi kuwa kuna wachezaji
ambao uwezo wao ni mdogo hivyo inabidi wawatoe kwenye dirisha dogo la usajili,
lakini ukiwa na wachezaji wazuri wenye kuonesha uwezo na wanataka kucheza kuisaidia
timu yao sioni kwanini asiwachukue kwa vile bado hajamaliza usajili wote.
Pia alisema usajili wa wachezaji wa kigeni
unaofanywa na baadhi ya klabu hapa nchini haumtishi kwani yeye ni kocha mkubwa
na anatambua uwezo wa wachezaji wengi na hata pale anapowaita wachezaji anaangalia
uwezo wa mchezaji na si umri.
“Mimi
sitishiki na usajili wa Azam, Simba na Yanga, wao wamevutika na wachezaji wa nje
kwasababu zao binafsi na kwa sababu wana fedha pia Yanga wanatarajia wakiwa na
wachezaji wa kigeni watafanikiwa kwasababu wanacheza mashindano ya Afrikahivyo
wanataka kuingia kwenye nane bora ‘Super eight’ lakini sidhani kama hilo
litafanikiwa”, alisema Julio
Pamoja na maneno mengi Julio alionesha
kuukubali usajili wa Azam na kusema juzi
wamefanya vizurui kuchukua ubingwa na kukiri timu hiyo sio mbaya lakini akasema
Simba wao wanataka kuchukua ubingwa ambao wameupoteza kwa takribani miaka mitatu
No comments:
Post a Comment