Blandina Patrick |
WANARIADHA
watano wa timu ya Olimpiki Maalum inayoshiriki mashindano ya dunia
yanayofanyika Marekani wamepata medali.
Akizungumza
kwa njia ya mtandao kutoka Los Angels, Marekani jana, Mkuu wa msafara, Frank
Macha alisema Tanzania imeendelea kujinyakulia medali baada ya juzi kupata
medali tatu.
Wachezaji wetu wamefanikiwa kupata medali
nyingine tano baada ya zile tatu ambazo zilinyakuliwa awali. Waliopata
medali ni Blandina Patrick amepata medali ya dhahabu na Deonatus Manyama medali ya fedha wote kwenye mbio za mita 800.
Wengine ni Faraja Meza aliyepata medali ya dhahabu, Riziki Chilumba
medali ya fedha na Aisha Kaoneka medali Shaba
kwenye mbio za mita 100 wote.
Wachezaji wengine ambao walishajinyakulia
medali ni Godfrey Jabuya, Blandina Patrick na Deonatus Manyama kwenye mbio za
mita 400 hivyo hadi sasa Tanzania imefikisha
jumla ya medali nane, dhahabu tatu, fedha tatu na shaba mbili
Timu
hiyo ina wachezaji wanane, wanawake wanne na wanaume wanne, itashiriki katika
mchezo wa riadha katika mita 100, 200, 400, 800, 5000, nusu marathon na mita
4x100 kupokezana vijiti. (Relay).
No comments:
Post a Comment