Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, July 31, 2015

SHILOLE AFUNGIWA MWAKA MMOJA NA BASATA, KISA HIZI PICHA



 
 
BARAZA la sanaa Tanzania (BASATA) limemfungia mwanamuziki Zuwena Mohamed ‘Shilole’  kutojihusisha na kazi yoyote ya sanaa kwa muda wa mwaka mmoja ndani ya nchi na nje.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Shilole kucheza uchi wakati akiwa jukwaani nchini Ubelgiji na picha zake kusambaa kwenye mitandao.
Katika barua ambayo imetoka BASATA na kusainiwa na Katibu Mtendaji, Geofrey Mngereza  inasema “Mei  9 , 2015 ukiwa katika onyesho lako la muziki Ubelgiji ulicheza uchi mbele ya hadhira ya wapenda sanaa za Tanzania hivyo kudhalilisha utu wako na jamii ya kitanzania kimaadili”
Mngereza aliendela kusema BASATA ilimpa nafasi ya kutoa maelezo kwanini asichukuliwe hatua za kinidhamu kwa tabia hiyo lakini alikaidi kutoa maelezo hivyo BASATA imejiridhisha kuwa umekiuka maadili ya kazi za sanaa kwa makusudi na umekiuka sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji sanaa.
Pia iliendelea kusema kuwa “BASATA octoba 2013, ilikuonya na ukakiri kwa kuomba msamaha tabia yako ya kucheza bila kuzingatia maadili unapokuwa jukwaani.
Mngereza alisema Shilole amekiuka amekiuka sheria kwenye ibara ya 30 (2)(b) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa kuvunja maadili ya jamii ya Mtanzania pia amekiuka sheria Na. 23 ya mwaka 1984 ya BASATA kifungu cha 4 (i) kinacholipa baraza wajibu wa kusimamia kazi zote za sanaa na kanuni ya 26(20 (b) ya kanuni za baraza G.N 322 za Octoba 21, 2005 kwa kucheza uchi mbele ya hadhira.
Baraza limesimamisha kujishughulisha na kazi za sanaa nchini na nje ya nchi kwa mwaka mmoja, kufanya kinyume na hayo kutasababisha kupewa adhabu zaidi pamoja na yeyote utakayeshirikiana naye kuanzia Julai 24, 2015 hadi pale itakavyoamuliwa vinginevyo.

No comments:

Post a Comment