RAIS
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi ametuma salam za
pongezi kwa klabu ya Azam FC kwa kufanikiwa kuingia katika hatua ya nusu
fainali ya michuano ya Kombe la Kagame inayotimua vumbi jijini Dar es salam.
Katika
salamu zake kwa uongozi wa klabu ya Azam, Malinzi amewataka kutobweteka na
kuongeza bidii katika hatua hiyo ya nusu fainali ili waweze kufuzu kwa hatua ya
fainali na kutwaa Ubingwa na kuwaomba watanzania wote kuwasapoti wawakilishi
pekee wa nchi kwenye michuano hiyo
TFF
kwa niaba ya familia ya mpira na watanzania wote, inatwakia kila la kheri Azam
FC katika mchezo wake wa leo wa nusu
fainali dhidi ya KCCA.
No comments:
Post a Comment