Timu ya Simba leo imekubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliochezwa jioni katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Bao la Mtibwa Sugar, limefungwa na Mshambuliaji Salvatory Ntebe, katika dakika ya 19, baada ya kuwatoka mabeki wa Simba na kumchambua kipa Juma Kaseja.
Bao hilo limedumu hadi kumalizika kwa mchezo huo, jambo ambalo limezua mtafaruku mkubwa baina ya Mashabiki, Wanachama wa timu ya Simba, walikuwa wakishinikiza kutaka kuonana na viongozi wao ili kuzungumza falagha kuwashinikiza kuitisha mkutano mkuu wa dharura.
Hata hivyo mashabiki hao na wanachama wa Simba, waligoma kuondoka uwanjani hapo hadi walipotawanywa na gari la Polisi lililoanza kurushia maji ya kuwasha, huku vingozi wa timu hiyo na wachezaji wakiwa wamefungiwa ndani hadi kundi la watu hao lilipotawanywa na viongozi na wachezaji kusindikizwa na askari wa kutuliza ghasia (FFU)
Hata hivyo katika mchezo huo Beki wa Simba, Juma Nyoso, alipewa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Vicent Barnabas, katika dakika ya 85.
No comments:
Post a Comment