Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, April 17, 2015

EDEN HAZARD, DIEGO COSTA KWENYE LISTI YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA


Diego Costa na Eden Hazard wameiongoza Chelsea kufikia ilipo mpaka sasa Kileleni kwenye Ligi Kuu England BPL Na sasa wapo kwenye Listi ya Wachezaji 6 wanaowania Tuzo hiyo.Straika wa England Harry Kane mwenye goli 19 mpaka sasa, Listi hiyo inahusishwa pia kuwemo Philippe Coutinho, Kipa wa Manchester United David de Gea na Mchezaji wa Arsenal fowadi Alexis Sanchez.
Luis Suarez ndie aliyekuwa mshindi wa Tuzo hiyo msimu uliopita na sasa akikipiga kwenye Klabu la Barcelona na jana amefunga bao mbili kwenye Klabu Bingwa Ulaya.
Tuzo hiyo itatolewa mwezi huu April 26.
Harry Kane - SpursEden Hazard - ChelseaAlexis Sanchez - ArsenalDiego Costa - ChelseaDavid De Gea - Man United.
PFA, Professional Footballers' Association, Chama cha Wachezaji wa Kulipwa wa England, kila Mwaka hutoa Tuzo hizi za Madaraja mawili, zile za Wakubwa na Vijana, na hao Wanne wanagombea Tuzo zote mbili kwa mpigo kwa vile Umri unawaruhusu na pia sababu ya ustadi wao.
Pamoja na Kane, Coutinho, Hazard na De Gea, kugombea Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka, pia wapo Winga wa Arsenal, Alexis Sanchez, na Straika wa Chelsea, Diego Costa.
Kwenye Tuzo ya Mchezaji Bora Kijana, hao Wanne watajumuika na Kipa wa Chelsea, Thibaut Courtois, na Fowadi wa Liverpool, Raheem Sterling, kuiwania.
Kwa Eden Hazard, hii ni mara ya 3 kugombea Tuzo hii baada ya kubwagwa na Gareth Bale na Luis Suarez.
Ikiwa David De Gea atatwaa Tuzo hii, basi itakuwa mara ya kwanza kwa Golikipa tangu Kipa wa England, Peter Shilton, kuitwaa Mwaka 1977.

(PFA) WACHEZAJI BORA WANAOWANIA TUZO HIYO YA MWAKA NI:-
1. Eden Hazard

2. Harry Kane
3. Alexis Sanchez
4. David De Gea

5. Philippe Coutinho
6. Diego Costa

MCHEZAJI BORA KIJANA WA MWAKA

Thibaut Courtois (Chelsea)
Philippe Coutinho (Liverpool)
David De Gea (Manchester United)
Eden Hazard (Chelsea)
Harry Kane (Tottenham Hotspur)
Raheem Sterling (Liverpool)

No comments:

Post a Comment