UTANGULIZA
Karibuni
sana kwenye mkutano maalumu wa ufunguzi wa mashindano ya Sports xtra Ndondo cup
2018, ikiwa ni msimu wake wa tano tangu kuanzishwa kwake mwaka 2014.
Kama
mnavyofahamu Ndondo CUP inahusisha timu za mitaani tunakotoka na lengo lake
mama ni kuwapa nafasi vijana wenye vipaji vya kucheza mpira kuweza kuonekana na
wadau wengine kama ambavyo Clouds Media tunavyosema tunakufungulia dunia kuwa
unachotaka.
Sasa kwa
misimu yote minne tumekua na mabadiliko katika kila msimu ya uboreshaji na
kuifanya Ndondo CUP kuwa maisha halisi ya mtanzania katika kila angle mbali tu
na kuchezwa mpira bali tutaangali vyakula vyetu, music wetu, na tabia zetu kwa
ujumla, tunasema (life style) ya
uswahilini kwetu.
Msimu wa tano
tunataka kuwekeza zaidi katika mtazamo huo, mpira wa miguu kwa maana ndani ya
uwanja iwe asilimia 40 tu, lakini asilimia 60 zinazosalia iwe ni mambo mengine
yaliyo nje ya uwanja kama nilivyoeleza hapo awali.
Ndondo cup
iwe ni mtoko halisi unapokuja katika viwanja vyetu tunavyovitumia basi uwe na
uwezo wa kupata mahitaji muhimu kama chakula chetu cha kindondo mfano tu wali
maharage, miguu ya kuku, mihogo, uji wa mchele, pweza kidogo na mahitaji
mengine tunayoyapata hata tukiwa maskani mwetu.
Burudani ya music,
show za wasanii na ulinzi wa kutosha ni vitu ambavyo tumekua tukiishi navyo
tangu tulipoanza mwaka wa kwanza na yote mtakua mashahidi wa hili..
Ukuaji wa
mashindano haya nao hauko nyuma tulianza mwaka jana kwa kuongeza mikoa miwili
ya Mwanza na Mbeya na hivyo hivyo mwaka huu tutaendelea kuwa na mikoa mingine miwili
nje ya Dar es salaam.
Kwa
kushirikiana na vyama vya soka vya mikoa husika naamini tutafanikisha azma yetu
ya mpira kuchezwa na vijana wenye vipaji kuonekana.
Kwa maelezo
hayo mafupi leo tunazindua msimu mpya wa ndondo cup 2018 ukiwa na kauli mbiu
(slogan) "WASHTUE WANAAAA" kama ilivyokua utaratibu wetu.
Na mwaka huu
Ndondo Cup itafanyika mkoa wa Mwanza kama ilivyokua mwaka jana lakini pia tumeuongeza
mkoa wa Ruvuma ambao unachukua nafasi ya Mbeya .
KUHUSU USAJILI WA TIMU
Baada tu ya
kumalizika press hii zoezi la usajili wa timu kwa mkoa wa Dar es salaam utaanza
rasmi kupitia usimamizi wa chama cha soka mkoa huo (DRFA) kupitia kamati yake
ya mashindano kwa ada ya ushiriki kiasi cha shilingi laki tatu (300,000)/= ambazo
zitalipwa kupitia account ya DRFA.
Kwa wale wa
mikoani tutawajulisha zoezi la usajili wa timu utafanyika kuanzia lini, lakini
ada ya ushiriki itakua laki tatu (300,000) kwa mikoa yote.
ZAWADI
Kila mwaka tumekua
na maboresho katika zawadi inawezekana haikua ya fedha lakini kuna upande
mwingine kuna kitu kiliongezeka mfano mwaka jana tuliongeza tuzo maalum ambazo
sisi tunaamin ni muhimu sana kwa mchezaji.
Mwaka huu
hakutakua na ongezeko la fedha kwenye zawadi za mwisho itabaki kama ilivyokua
kwa bingwa milion kumi, mshindi wa pili milion tano na mshindi wa tatu milion
tatu lakini mwaka huu tumeongeza hadi mshindi wa nne atapata milion moja.
Lakini
tulichofanya ni kuboresha kwa kuzipa fedha ya maandalizi timu ambazo
zitafanikiwa kuingia hatua ya mtoano kuanzia 16 bora ambapo timu zote zitakazo
ingia hatua hiyo tutazipa laki tano kila moja kwa maandalizi.
Timu 8
zitakazoingia robo fainali tutazipa milion moja moja kwa ajili ya maandalizi ya
michezo yao hali kadhalika timu nne zitakazoingia nusu fainali nazo zitapewa
kiasi cha shilingi milion moja na nusu kwa kila mmoja kwa ajili ya maandalizi.
Na zile timu
mbili zitakazoingia fainal zitapewa milion mbili za maandalizi.
Ikipiga
hesabu vizuri utagundua timu itakayo kuwa bingwa itakua imekusanya milion 15
lakini hawa wengine nao watakua wamepata fedha.
Mbali na
zawadi ya fedha mwaka huu tutazipa timu usafiri kwa ajili ya wachezaji kuanzia
hatua ya 16 bora kuwapeleka uwanjani na kuwarudisha.
Lakini pia tunafahamu
changamoto zinazowakabili timu wakati wa maandalizi na kama nilivyosema toka
mwanzo ndondo inaenda hadi kwenye utamaduni wa chakula hivyo tumu zinazoingia
hatua ya 116 bora nazo tutazipa chakula cha mchana kwa wachezaji na viongozi wasiozidi
30.
Tutaendelea
kuwa na zawadi za mtu mmoja mmoja kwa maana ya mfungaji bora, mchezaji bora,
kipa bora, kocha bora, mchezaji chipukizi n.k
Kikundi bora
cha ushangiliaji zawadi yake itaendelea kuwa milion moja lakini tutakua na
zawadi ya shabiki mmoja mmoja ambazo zitakua kwa shabiki watano maana tumegundua
kuna mashabiki wanafanya vizuri lakini sio kundi na kukosa nafasi ya kupata
zawadi.
Utaratibu
huu wa zawadi ni kwa mkoa wa Dar es salaam pekee
ZAWADI MWANZA
Bingwa
atapata milion tano kutoka tatu za mwaka jana, mshindi wa pili milion tatu na
mshindi wa tatu milion mbili. Pia zawadi za mshindi mmoja mmoja itabaki kama
ilivyokua shilingi laki tano.
Bila kusahau
kikundi bora cha ushangiliaji ni milion moja
ZAWADI RUVUMA
Bingwa
atapata milion tatu, mshindi wa pili milion mbili na mshindi wa tatu milion
moja, mshindi mmoja mmoja watapata zawadi ya fedha shilingi laki tano.
Bila kusahau
kikundi bora cha ushangiliaji ni milion moja
WADHAMINI
Mwaka jana
kama tunakumbuka vizuri hatukua na mdhamini mkuu, lakini mwaka huu tupo na mCheza
Tanzania ambao ni kampuni ya mchezo wa kubashiri matokeo, tutakua nao pia BEKO ambao
ni watengenezaji wa vifaa vya kieletroniki vya majumbani, Macron watengenezaji
na wasambazaji wa vifaa vya michezo kutoka Italy, ambao watatoa vifaa kwa timu
32 shiriki hatua ya makundi, lakini pia watatuma mascout katika hatua ya 16
bora kwa ajili ya kuwapeleka katika klabu ya Bologna ya italia ambayo ipo chini
yao, bila kuwasahau Azam Tv ambao tumekua nao tangu mwaka wa kwanza wa
mashindano.
Pamoja na
kuwepo kwa hawa bado milango ipo wazi kwa wadau wengine kwa sababu bila nguvu
ya wadhamini ki ukweli changamoto ni nyingi.
UTARATIBU WA WAANDISHI WA HABARI (ACCREDITATION)
Kwa
waandishi wa habari tutaendelea na utaratibu wa kujisajili kwa njia ya mtandao
ili kupata access ya kuripoti au kuingilia uwanjani.
Na mwaka huu
tutajitahid kuboresha zaidi mazingira ya wana habari ili kuwapa nafasi ya kufanya
kazi zao kwa ufanisi.
RATIBA YA MASHINDANO
RATIBA YA MATUKIO YA
SPORTS XTRA NDONDO CUP 2018
NO.
|
TAREHE
|
TUKIO
|
ENEO
|
1.
|
9 March 2018
|
Press conference-Ufunguzi msimu
Kuanza kwa Usajili wa timu shiriki
|
Dar es
salaam (escape one)
Ruvuma
Mwanza
|
2.
|
6 April -
6 May 2018
|
Hatua ya awali
|
Dar es
Salaam
Viwanja....
v Kinesi
v Mabatini tandika
v Benjamini mkapa
v Ukombozi
v Airwing ukonga
v Bandari
|
3.
|
25
May 2018
|
v Hafla ya upangaji makundi 32 bora.
v Semina kwa viongozi wa timu shiriki.
v Ugawaji wa vifaa kwa timu na waamuzi.
|
Dar es
Salaam (escape 1)
|
4.
|
1 June -
22 Julai 2018
|
Hatua ya
32 bora....
v 1 - 24 june-Michezo ya makundi.
v 25 june-Droo ya 16 bora mtoano.
v 27 june -4 julai-Michezo ya 16 bora mtoano.
v 2 julai-Droo ya robo fainal.
v 6 - 9 julai - Michezo ya robo
fainal.
v 9 julai- Droo ya nusu fainal.
v 14 - 15 julai-Michezo ya nusu fainal.
v 20 julai - Mchezo wa mshindi wa tatu.
v 22 julai - Fainali Ndondo Cup
|
Dar es
Salaam
Viwanja....
v Bandari
v kinesi
|
5.
|
28 Julai
2018
|
Usiku wa tuzo za Ndondo Cup
|
Dar es
Salaam (clouds media)
|
|
|
|
|
6.
|
18 Aug -22
Sept 2018
|
Ndondo Cup mkoani Ruvuma
|
Songea
Mbinga
|
7.
|
5 Oct - 10
Nov 2018
|
Ndondo Cup Mkoani Mwanza
|
Mwanza
|
8.
|
15 - 22
Dec 2018
|
Ndondo Super Cup
|
Dar es
salaam
|
NDONDO ACADEMY
Almas Kasongo-m/kiti DRFA
Pamoja na
kuwepo kwa ndondo cup mwaka huu tumekusudia pia kuwepo kwa ndondo academy kwa
vijana wenye umri wa chini ya miaka 15 kutoka vituo mbalimbali vya michezo na
mashule ya jiji la Dar es salaam.
Michezo ya
mashindano haya itakuwa ikichezwa kila wikiendi na kipindi ambacho shule
zitakua zimefungwa basi tutayachezesha hadi katikati ya wiki.
Usajili wake
unaenda sambamba na usajili wa ndondo cup na ada yake itakua shilingi laki moja.
UDHAMINI WA mCHEZA TANZANIA
Moses Simon - Mkuu wa kitengo cha
masoka-mCHEZA
NapendakuchukuafursahiikuwashukuruwaandishiwahabariwotekwakufikahapailikuwezakuwahabarishaWatanzaniakuhusuufunguzihuurasmiwamashindanohayakwamwaka
2018 kupitia UDHAMINI MNONO KUTOKA Mcheza Tanzania.
KipekeekabisaMcheza Tanzania, tunawashukuruwaandaajinawaratibuwamashidanohayayaNdondo
Cup kampuniya Clouds media group kwaushirikianowa SHADAKA SPORTS MANAGEMENT
chiniyausimamizimzuriwaNduguShaffihDauda, lakinibilakuwasahau TFF.
Mcheza Tanzania
nikampunimpyayamichezoyakubashiriiliyosajiliwakisherianaBodiyamichezoyakubahatisha
Tanzania iliyopewaLesenihalalikwaajiliyakuendeshashughulizake Tanzania.
TumekuatukiyafatiliamashindanohayayaNdondo cup
kablahatahatujaanzashighulizetu, kamaMcheza Tanzania
maonoyetumakubwanikuibuavipajivyavijanawaliokomtaaniambaohawajawezakupatanafasiyakuoneshavipajivyaoiliviwezekuwasaidiakuendeshamaishayao.
KwahiyotulivutiwasananaMashindanohayakwasababuyalilengakusaidiakuibuavipajivyavijanawadogokabisawaliopomtaaniambaohawakuwahikupatafursayakuvioneshavipajivyaoambavyovingewezakuwamsaadanakuendeshamaishayaokupitiavipajihivyo.Lakini
pia kupunguzawimbikubwa la
vijanakujihusishanamatukioyakiuharifunabadalayakewajihusishenamichezoambayokwasasaniajiranzurikabisakwavijana.
Mwaka 2017 Mcheza Tanzania
tulidhaminimashindanohayakwamikoamitatuambayoni, Dar es salaam, Mwanza na
Mbeya. Vipajivingitulivionanamafanikioyalikuamakubwasana.
Mwaka 2018 namiakamingineinayokujaMcheza Tanzania
tumeamuakujanaudhaminimnono Zaidi ilikuongezathamaniyamashindanohaya,
tunatakazawadiziwenyingikwavipengerevingitofautitofautiilikuongezamorali
(motisha) kwawachezajinawashangiliaji pia.
Tunaziombatimuzotezitakazoshirikimashindanohayazidumishe
Amani naupendokama FIFA wanavyosema “FAIR PLAY”
Mwishokabisa tuna
wakaribishawotekujisajilinakubashirinamchezakupitiatovutiyetuya www.mcheza.co.tz
kuna Odds bomba, machaguo (options) zaidiya 200 kwamechimoja, Live betting,
bonasizaukweli, Malipoyapapokwahaponahudumakwawatejasaa 24 piganamba
0764701600. Jishindiemshikowakutosha,
Kwa habarimbalimbalitafadharitufatekwenyekurasazetuzamitandaoyakijamiiyotekwajina
la Mcheza TZ.
Mcheza “USHINDI
KOTE KOTE”
No comments:
Post a Comment