Mkufunzi George Komba (kulia) na Oscar Mirambo na Mhadhiri wa UDSM Albert Kimaro wakiteta jambo |
Wana kozi ya awali ya ukocha inayoendeshwa na KIFA kwenye viwanja vya Chuo Kikuu |
Mhadhiri wa UDSM, Albert Kimaro akifundisha kwa vitendo wakati wa kozi ya awali ya ukocha inayofanyika Viwanja vya chuo hicho |
WAHADHIRI wawili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
wanatarajia kufuzu mafunzo ya awali kozi ya ukocha inayoendeshwa na Chama cha
Soka, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Waadhiri hao ni Noel Kiunsi Albert Kimaro ambao wote
wapo Idara ya Physical Education ya Chuo hicho.
Akizungumza wakati wa mazoezi ya vitendo yanayofanyika
kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu, Noel Kiunsi alisema kuwa ameamua kujiunga na
kozi hiyo ili apate nafasi ya kufundisha vilabu vya mtaani kwani kutokana na
kanuni za Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) hazitambui watu wenye shahada ya
michezo kama ilivyo wao.
“Mimi nin shahada ya michezo lakini siwezi kufundisha
timu zinazoshiriki ligi ya TFF bila kuhudhuuria kozi ambazo wanaendesha wao ndo
maana nimejiunga ili nitumie ujuzi hadi nje ya chuo”, alisema Kiunsi.
Kozi ambayo
imeandaliwa na Chama cha Soka Mkoa wa Kisoka Kinondoni (KIFA) inafundishwa na
Mkufunzi George Komba toka Dodoma akisaidiana na Oscar Mirambo.
Jumla wa makocha 23 wanatajia kutunikiwa vyeti vya
awali endapo watafauli mitihani ya nadharia na vitendo kwenye kozi hiyo ambayo
ilianza Februari 16 na inatarajiwa kumalizika kesho.
No comments:
Post a Comment