Rais Malinzi akiongea na wandishi kushoto ni Mkurugenzi wa Mashindano, Boniface Wambura na kulia ni mshauri wa rais wa mambo ya ufundi |
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF)
limetoa agenda za mkutano wake Mkuu utakaofanyika mjini Morogoro kati ya Machi 14,15 mwaka huu katika
Ukumbi wa Morogoro Hotel
Akizungumza na wandishi wa
habari , Afisa habari wa Shirikisho la Soka nchini
(TFF), Baraka Kizuguto alisema kuwa mkutano utafanyika mjini Morogoro na
mandalizi yanaendelea vizuri
“Kama mnavyojua
TFF itafanya mkutano wake Mkuu Machi 14 na 15 mwaka huu mjini Morogoro na
maandalizi yanaendelea vizuri”, alisema Kizuguto.
Agenda za mkutano mkuu ni kufungua Mkutano, uhakiki
wa Wajumbe, kuthibitisha Ajenda,
kuthibitisha Muhtsari wa Mkutano Mkuu uliopita na yatokanayo na Mkutano
uliopita.
Nyingine ni hotuba ya Rais, ripoti kutoka kwa
Wanachama, kuthibitisha ripoti ya
utekelezaji wa Kamati ya Utendaji, kuthibitisha ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu
2013.
Pia kutakuwepo na agenda ya kuthibitisha ripoti ya
Kamati ya Ukaguzi wa Hesabu, kupitisha bajeti ya 2015, marekebisho ya Katiba, mengineyo na mwisho ni kufunga
Mkutano.
Awali Mkutano huu ulikuwa ufanyike mkoani Singida
lakini ulihamishwa kutokana na mkoa huo kutokuwa na hoteli za kukidhi mahitaji
ya wajumbe na gharama kuwa juu.
No comments:
Post a Comment