TABIA ya Bodi ya Ligi kubadilisha ratiba imeendelea
kuota mizizi ambapo jana imetangaza tena kuharishwa kwa michezo miwili ya Ligi
Kuu Tanzania Bara ambayo iliyokuwa ichezwe leo.
Akizungumza na wandishi wa Habari, Afisa Habari wa
Shirikisho la Soka Nchini, (TFF) Baraka Kizuguto alitangaza kuahirishwa kwa
michezo ya JKT Ruvu dhidi ya Young Africans katika uwanja wa Taifa, na Mgambo
Shooting dhidi ya Azam FC uwanja wa Mkwakwani jijini.
Kizuguto alisema michezo hiyo ambayo ilikuwa ichezwe
leo sasa itapangiwa tarehe nyingine bila
kutoa sababu za kuhahirishwa.
Katika kutaka kusikia maoni ya wadau wa soka gazeti
hili lilimtafuta meneja wa Azam FC Jemedariambaye alikuwa na haya ya kusema
“Sisi tulikuwa
tuondoke leo kwenda Tanga lakini cha kushangaza usiku tulipata taarifa toka
BodI ya Ligi kuwa tusiende Tanga kwani mchezo huo umeharishwa na badala yake
tujiandae na mchezo dhidi ya Ndanda FC ambao tutacheza jumamosi”, alisema
Jemedari
Awali Yanga walilalamika mchezo huo dhidi ya JKT Ruvu
kusogozwa mbele ambapo awali ulipangwa kuchezwa Machi 4, mwaka huu kudai
watakosa muda wa kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao wanatarajia
kucheza Machi 14 mwaka huu.
Wadau wa soka wamelalamikia kitendo cha ratiba ya ligi
kupanguliwa kila mara ambapo hadi sasa imeshapanguliwa mara tatu bila sababu za
msingi na kusema ratiba hiyo haieleweki zaidi inavuruga timu.
No comments:
Post a Comment