Bondia Mada Maugo amemaliza ubishi kwa
kumtwanga Japhet Kaseba kwa KO.
Maugo amemchapa Kaseba katika raundi ya nane
katika pambano lililomalizika muda mfupi uliopita kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,
Dar.
Pambano hilo lilikuwa la kumaliza ubishi
kati yao na Maugo alitawala raundi mbili za mwanzo, kabla ya Kaseba kutawala
raundi ya tatu na nne.
Kaseba alishindwa kuvumilia mapigo ya Maugo
baada ya kuchapwa kwa konde kali la kushoto na kuanguka katika raundi ya nane.
Katika pambano jingine, Karama Nyilawila naye alimshinda Ibrahim Tambwe kwa KO katika raundi ya pili.
No comments:
Post a Comment