Kocha Bakari Shime |
KOCHA wa
Mgambo Shooting ya Handeni Tanga, Bakari Shime, amesema
anatarajia timu itafanya vizuri kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Ndanda Fc
utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Mgambo ambao watakuwa wenyeji wa Ndanda FC wanaingia
uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 na Coastal Union kwenye
Uwanja huo wa Mkwakwani.
Shime alisema kuwa timu yake ipo vizuri
kisaikolojia na kiufundi pia na makosa ambayo yalijitokeza kwenye mchezo
uliopita ameyafanyia marekebisho.
“Timu imejiandaa vema na tuna imani tutaondoka
na pointi tatu japo pia wapinzani wetu si wa kubeza kwani mchezo utakuwa wa
ushindani”, alisema Shime.
Mgambo Shooting inashika nafasi ya 13 ikiwa na pointi 17 ikiwa imeshacheza michezo
15 kwenye ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2014/15 na Ndanda FC inashika nafasi
ya saba ikiwa na pointi 22 na imecheza michezo 17.
Ndanda wataingia uwanjani wakiwa na
kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 2-1 waliopata ugenini dhidi ya Ruvu
Shooting ya Pwani kwenye mechi iliyopita.
Michezo
mingine kesho ni Mbeya City wataokuwa wageni wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa
Manungu Turiani huku Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam watani wa jadi Simba
SC watakuwa wenyeji wa Young Africans, mchezo unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi
majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment