KATIKA
kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani, Asia Idarous ameandaa ‘Usiku wa Mwanamke’
utakaofanyika kesho ndani ya ukumbi wa Safari Carnival uliopo Mikocheni B, Jijini
Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Mtendaji Mkuu wa Fabak Fashins, Asia Idarous Khamsin aliwaomba Wanawake kujitokeza kwa wingi usiku huo maalum kwani ni usiku wao na utakuwa na mambo mbalimbali ikiwemo burudani ya taarabu kutoka kwa bendi ya Gusa Gusa

“
Nawakaribisha wanawake wote ndani ya Safari Carnival tusheherekee siku yetu
huku tukiwa tumevalia kiafrika zaidi lakini pia wanaume wanatakiwa waje
kuungana nasi”, alisema Asia.
Pia alisema kiingilio
ni 10,000/= na kutakuwepo na zulia jekundu kwa ajili ya picha za kumbukumbu
litakalopambwa na wabunifu na wanamitindo mbalimbali.
Pia alisema
kutakuwepo waimbaji nguli wa taarabu, Sabaha Muchacho, Afua Suleiman
na Shakila ambao wanatarajiwa kutoa burudani ambayo itanogesha siku ya
wanawake
Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa kila mwaka Machi 8 ambapo mwaka huu ujumbe unasema ‘Uwezeshaji wanawake, Tekeleza wakati ni huu’
No comments:
Post a Comment