Kocha Juma Bomba wa timu ya Sayari Wanaume, akiongea na wachezaji wake wakati wa mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Msimbazi Rovers Ilala, jijini Dar es Salaam |
KOCHA
wa timu ya soka la wanawake ya Sayari
Women Sports Club, Juma Bomba amewataka wasichana wanaopenda kujifunza mpira wa
miguu kujitokeza.
Bomba
aliyasema hayo jijini na kusema kuwa Sayari inahitaji kuwa na wachezaji wengi
chipukizi hivyo wale wote wanaopenda kujifunza wanakaribishwa wafike Uwanja wa
Msimbazi Rovers, Ilala kuanzia saa 10:00 jioni siku za Jumatatu hadi Ijumaa.
“Nimejitolea
kuwafundisha soka bure hivyo wasichana wote wanakaribishwa wafike siku ya
Jumatatu hadi Ijumaa saa kumi jioni”, alisema Bomba
Pia
anasema Sayari wanaanzisha timu ya soka la Ufukweni kwa wasichana hivyo wachezaji
watakuwa na fursa ya kucheza michezo mingi wakiwa Sayari.
Juma
pia amewataka viongozi wa soka Mkoa wa Dar es Salaam kusimamia kikamilifu soka
na kuhakikisha ligi ya wanawake inachezwa kwani linaelekea kupoteza mwelekeo
baada ya kusimama kwa misimu miwili bila kuchezwa.
Sayari
ni moja timu kongwe kwenye soka la wanawake chini ya Mwenyekiti Fatuma Mkambara
na imeshawahi kutwaa Ubingwa wa soka la wanawake Mkoa wa Dar es Salaam mara
kadhaa.
No comments:
Post a Comment