Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, March 20, 2015

HOWARD WEBB KUPANGA WAAMUZI MECHI ZA LIGI KUU ENGLAND

REFA mahiri wa zamani wa England aliewahi kuchezesha Fainali ya Kombe la Dunia Mwaka 2010, Howard Webb, sasa ndie mwenye jukumu la kupanga Marefa wanaochezesha Mechi zote za Ligi Kuu England.
Tangu astaafu Urefa Mwaka Jana, Webb amekuwa ni Mkurugenzi wa Ufundi wa PGMOL, Professional Game Match Officials Limited ambacho ni chombo kinachosimamia Marefa huko England.

PGMOL, chini ya Refa wa zamani Mike Riley ambae ndie Meneja Mkuu, sasa kimempa wadhifa mpya Howard Webb wa Mkurugenzi wa Uendeshaji na moja ya majukumu yake ni kupanga Marefa kwa kila Mechi za Ligi Kuu England. Ligi Kuu England inalo kundi maalum la Marefa spesho tu kwa Mechi zake tu na hao idadi yao ni 17.

No comments:

Post a Comment