KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Uganda ya The Cranes, Micho
Sredojevic ametangaza kikosi cha wachezaji 25 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo
wa kimataifa wa ugenini dhidi ya Nigeria huku Emmanuel Okwi wa Simba akimuweka
kando.
Okwi anayeichezea Simba ya Tanzania kwa sasa yuko katika
kiwango cha juu baada ya kuifungia timu yake bao pekee walipoichapa Yanga 1-0
kabla ya kufunga dhidi ya Mtibwa.
Wakati Micho akimuacha Okwi, wachezaji wengine wanaocheza
soka Tanzania wameitwa akiwemo Brian Majwega wa Azam FC na Jjuko
Murushid wa Simba.
The Cranes itaikabili Super Eagles Jumatano ya wiki ijayo
huko Akwa Ibom katika moja ya mechi kibao zitakazochezwa katika kalenda ya
Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) wiki ijayo.
Kikosi kina makipa wanne, mabeki nane, viungo tisa na
washambuliaji wanne.
Kipa Dennis Onyango, beki Isaac Isinde, kiungo Kizito
Luwagga na mshambuliaji Geoffrey Massa ni miongoni mwa baadhi ya wachezaji
wenye uzoefu walioitwa katika kikosi hicho cha Micho, ambao wote walikuwemo
katika kikosi kilichoshindwa kufuzu kwa Mataifa ya Afrika 2015.
Beki Savio Kabugo hayumo kutokana na maumivu wakati nahodha
Andy Mwesigwa ataukosa mchezo huo.
Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi naye pia hayumo katika
kikosi licha ya mchezaji huyo kuonesha makali yake katika kikosi cha Simba hivi
karibuni walipocheza dhidi ya Yanga.
Kwa mara ya mwisho Uganda na Nigeria zilikutana mwaka 2007
katika mechi za kufuzu kwa fainali za Kombela Mataifa ya Afrika za 2008 huku
Uganda ikiondoka na ushindi wa 2-1 katika mchezo uliofanyika Kampala na
kufungwa 1-0 na Super Eagles ugenini huko Abeokuta.
Makipa: Dennis Onyango (Mamelodi Sundowns-Afrika Kusini),
Robert Odongkara, (St. George FC-Ethiopia), Jamal Salim (El Merreikh-Sudan),
Ismail Watenga (Vipers FC –Uganda)
Mabeki: Isaac Isinde (St. George- Ethiopia), Jjuko Murushid
(Simba SC-Tanzania), Richard Kasagga (Salam Zgharta-Lebanon), Joseph Nsubuga
(Bright Stars –Uganda), Ibrahim Kiyemba (Lweza FC-Uganda), Bakaki Shafiq
(Express FC-Uganda), Alex Kakuba (Estoril Praia-Portugal) na Godfrey
Walusimbi (Gor Mahia- Kenya)
Viungo: Dennis Guma (Al Ahed- Lebanon), Khalid Aucho (Gor
Mahia -Kenya), Kizito Keziron (Vipers FC-Uganda), Derrick Tekwo (Kira Young),
Mike Azira (Seattle Sounders-Marekani), Chrizestom Ntambi (SC Villa-Uganda),
Brian Majwega (Azam FC- Tanzania), Kizito Luwagga (Sporting Covilha –Ureno) na Farouk Miya (Vipers FC- Uganda)
Washambuliaji: Geoffrey Massa (Pretoria University –Afrika Kusini), Brian Umony (Saint George FC-Ethiopia), Robert
Ssentongo (URA FC-Uganda) na Patrick Edema (Beira Mar-Ureno)
No comments:
Post a Comment