CHELSEA WAIBUKA MABINGWA WA CAPITAL ONE CUP BAADA YA KUIFUNGA TOTTENHAM MABAO 2-0
CHELSEA
leeo hii Uwanjani Wembley Jijini London wametwaa Taji la kwanza la
Msimu, likiwa Kombe la kwanza kwa Meneja wao Jose Mourinho tangu 2012,
walipoichapa Tottenham Bao 2-0 katika Fainali ya Kombe la Ligi huko
England ambalo sasa linaitwa Capital One Cup. Kipindi
cha Kwanza Tottenham walitawala lakini Chelsea walipata Bao lao la
Kwanza Dakika ya 45 kutokana na Frikiki ya Willian kushindwa kuokolewa
na Beki wa Spurs Danny Rose ambae Kichwa chake duni kilimfikia John
Terry aliepiga Mpira uliomgonga Harry Kane na kumbabaisha Kipa wao Hugo
Lloris na kutinga. Dakika
ya 56 Chelsea walipata Bao lao la Pili baada ya Shuti la Diego Costa
kumbabatiza Beki wa Spurs Kyle Walker na kumhadaa Kipa Hugo Lloris. Kwa
kutwaa Capital One Cup Chelsea wanahakikishiwa kucheza Ulaya Msimu ujao
kwenye UEFA EUROPA LIGI lakini kama watamaliza kwenye 4 Bora za Ligi
Kuu England watacheza UEFA CHAMPIONS LIGI badala yake.
No comments:
Post a Comment