MARA
ya mwisho kukutana ni Mwezi uliopita Januari Mosi Uwanjani White Hart
Lane kwenye Mechi ya Ligi Kuu England na Tottenham Hotspur wakaibamiza
Chelsea Bao 5-3 lakini safari hii Wikiendi hii wapo Wembley Jijini
London kwenye Fainali ya Kombe la Ligi, Capital One Cup, hapo Jumapili.Siku
hiyo ya Mwaka Mpya, Straika hatari na Chipukizi wa Tottenham Harry
Kane, aliiongoza Spurs kwa kupiga Bao 2 na kutengeneza nyingine lakini
Beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic, amedai safari hii washapata dawa ya
kuitandika Chelsea kwenye Fainali.
Ivanovic amedai Chelsea, ambayo itamkosa Kiungo wao Nemanja Matic aliefungiwa Mechi 2, inao uzoefu wa kucheza Fainali kupita Spurs.
Ametamba: “Tunajua nini tunapaswa kufanya. Ni Gemu ngumu lakini tupo tayari na tunaingojea kwa hamu!”
Tottenham wametinga Fainali baada ya kuitoa Sheffield United kwa Jumla ya Mabao 3-2 kwa kushinda Mechi ya Kwanza wakiwa kwao White Hart Lane 1-0 kwa Bao la Penati ya Andros Townsend na kisha kutoka Sare 2-2 katika Marudiano Nyumbani kwa Sheffield United.Nao Chelsea walitinga Fainali baada ya kuifunga Liverpool 1-0 kwa Bao la Dakika za Nyongeza 30 la Branislav Ivanovic wakiwa Stamford Bridge baada ya Sare ya 1-1 katika Mechi ya Kwanza huko Anfield na kutinga Fainali kwa Jumla ya Mabao 2-1.

No comments:
Post a Comment