VAN GAAL ACHEKELEA TYLER BLACKETT KUSAINI MKATABA HADI 2017
Mkataba wa Mchezaji huyo mwenye Miaka 20 ambae alianzia kucheza kwenye Chuo cha Soka cha Man United tangu akiwa na Miaka Minane ulikuwa umalizike mwishoni mwa Msimu huu.
Mara baada ya habari hizi za Blackett kuibuka, Van Gaal alisema: “Nimefurahishwa sana kwa Tyler kusaini Mkataba mpya. Yeye ni mmoja wa Wachezaji Chipukizi ambao Msimu huu wameweza kuchezea Timu ya Kwanza. Tyler ana uwezo mkubwa wa kuendelea zaidi na naamini yupo Klabu sahihi itakayokuza maendeleo yake na kuwa Beki bora!”
Blackett, ambae amekulia Kitongoji cha Hulme ambacho kipo Maili 2 tu toka Old Trafford, amesema: “Nimefurahishwa mno kusaini Mkataba mpya. Nimekuwa Shabiki wa United maisha yangu yote na nipo hapa tangu nina Miaka 8. Kuanzia Chuoni na kuweza kucheza Timu ya Kwanza ni ndoto iliyotimia. Nataka nijiendeleze zaidi na Timu ya Kwanza kwa msaada wa Meneja, Makocha na Wachezaji wenzangu.”
Mapema Mwezi huu, Kinda mwingine wa Man United ambae pia alianzia Chuo cha Soka cha Man United, Paddy MacNair, alipewa Mkataba mpya.
Post a Comment