Mechi
za Marudiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 za EUROPA LIGI zimechezwa
Usiku huu na Klabu za England, ukiondoa Everton ambayo imeshinda Mechi
zao zote mbili kwa kishindo na kufuzu, Tottenham na Liverpool, zote
zimetupwa nje pamoja na Celtic ya Scotland.

Wachezaji wa Besiktas wakishangilia huko Uturuki leo
Liverpool,
ambao walishinda Mechi yao ya kwanza huko Anfield Wiki iliyopita, Leo
wamechapwa Bao 1-0 na Besiktas huko Uturuki na Mechi kwenda Dakika 30 za
Nyongeza lakini Matokeo yakabaki hivyo hivyo na ikaja Mikwaju ya Penati
5 na Besiktas kushinda 5-4.
Dejan Lovren ndie aliekosa Penati muhimu ya Liverpool. 
Dejan akipagawa baada ya kukosa mkwaju wa penati muhimu...

Umetukosesha ulaji Kijana!!

Dejan akiwaza!!

Daaa!!! leo! mhhh!

Nimekosa penati!!

Demba Ba furaha tupu!!

Wachezaji wa Besiktas wakishangilia huko Uturuki leo

Ushindi kwa Mikwaju ya penati!

Mapema penati zikipigwa Wachezaji wa Liverpool wakijiaminia

Tolgay ndie aliewafungia bao 1-0

Sahan akishangilia bao

Patashika kwa kipa wa Liverpool.
Nao
Tottenham, wakicheza Ugenini baada ya Sare ya Nyumbani ya 1-1,
walipigwa Bao 2-0 na Fiorentina huko Italy kwa Bao za Kipindi cha Pili
za Mario Gomes na Mchezaji wa Chelsea Mohamed Salah.
Celtic,
wakicheza Ugenini baada ya Sare ya Nyumbani ya 3-3 na Inter Milan,
walitandikwa Bao 1-0 huko San Siro Milan, Italy kwa Bao la Freddy Guarin
la Dakika ya 88.
Everton, ambayo ilipata ushindi mnono wa Ugenini
Wiki iliyopita walipoichapa BSC Young Boys ya Uswisi Bao 4-1, Leo huko
kwao Goodison Park wameitandika tena Young Boys Bao 3-1.
Bao za
Everton zilifungwa na Romelu Lukaku, Bao 2 moja la Penati, na jingine la
Kevin Mirallas huku Bao la Young Boys likifungwa na Sekoiu Junior
Sanogo.
Nao
Mabingwa Watetezi Sevilla wamesonga baada ya kuifunga Borussia
Mönchengladbach 3-2 huko Germany na hiki ni kipigo cha Pili kwa
Wajerumani hao baada ya pia kuchapwa 1-0 katika Mechi ya Kwanza.
Washindi
wa Raundi hii watajua Wapinzani wao Raundi ya Mtoano ya Timu 16 wakati
Droo ya Mechi zao itakapofanyika Leo Ijumaa Mchana huko Nyon, Uswisi.
The
last 16 are: EVERTON, Ajax, Besiktas, Club Brugge, Dinamo Moscow,
Dnipro, Dynamo Kiev, Fiorentina, Inter Milan, Napoli, Roma, Sevilla,
Torino, Villarreal, Wolfsburg, Zenit St Petersburg.
Post a Comment