Klabu hiyo maarufu ya Mjini Mbeya ambayo ni tishio Ligi Kuu Vodacom imetangaza habari hizi hii Leo.
Kwa mujibu wa Taarifa maalum ya Mbeya City Mkataba huo wa udhamini upo katika maeneo makubwa mawili ambayo ni vinywaji, yaani Maji aina ya Dasani wakati wa mazoezi na mashindano, pamoja na vinywaji vingine kulingana na mahitaji ya Klabu vitakavyokuwa na thamani ya Shilingi Milioni 15 na pia Fedha taslimu Shilingi Milioni 60 kwa Mwaka.
Taarifa hiyo ya Mbeya City imetoa shukrani kubwa kwa Kampuni ya COCA-COLA KWANZA kwa imani yao kwao na wao wameahidi kuongeza bidii ili wao na Wanamichezo wengine Nchini wanufaike kwa fursa za aina hii.
Mbiu ya Mbeya City sasa ni:
“Mbeya City timu yetu, RB Battery bidhaa yetu, CocaCola kinywaji chetu”
“Yes we Can”
No comments:
Post a Comment