Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, October 3, 2014

JI-SUNG PARK KUTAMBULISHWA RASMI JUMAPILI BAADA YA KUTEULIWA KUWA BALOZI WA OLD TRAFFORD!!


KIUNGO wa zamani Manchester United Ji-sung Park ameteuliwa kuwa Balozi wa Klabu hiyo.
Park, anaetoka Korea ya Kusini na mwenye Miaka 33, anaungana na Malejendari wengine wa Man United, kama vile Sir Bobby Charlton na Sir Alex Ferguson, kuwa Balozi wa Klabu hiyo maarufu Dunia nzima.

Park atatambulishwa rasmi kwa umati wa Old Trafford Jumapili kabla ya Mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Everton na kwenye shughuli hiyo ataambatana na Sir Alex Ferguson.

Akiongea kupitia Tovuti ya Man United, Park amesema: “Nina kumbukumbu nzuri sana ya wakati wangu nikiwa na Manchester United na nimefurahi na kupata heshima kubwa kuwa Balozi Klabuni hapa.”
Park (centre, left) celebrates winning the 2009 Premier League title, one of eight major honours he won during his time at Old Trafford 
Aliongeza: “Miongoni mwa kumbukumbu nzuri maishani mwangu ni zile zilizotokea hapa na sitasahau sapoti niliyopata toka kwa Klabu na Mashabiki. Nangojea kwa hamu kuiwakilisha tena United na kushirikiana na Wadau wetu wote Dunia nzima. ”
The midfielder left Old Trafford in 2012 to join QPR but he struggled with injuries at Loftus Road
Ji-sung Park aliichezea Man United kwa Miaka 7, kuanzia 2005 na 2012, na kushinda Ubingwa wa England mara 4, UEFA CHAMPIONS LIGI, Kombe la Ligi mara 3 na Kombe la FIFA la Klabu Bingwa Duniani.

No comments:

Post a Comment