Pierre Kwizera akiwasili leo |
KIUNGO mshambuliaji
wa kimataifa wa Burundi, Pierre Kwizera anamewasili nchini leo akiwa na
matumaini kibao ya kuisaidia Simba katika msimu ujao.
Kwizera
ambaye amewasili majira ya saa nane na ndege ya Shirika la Ndege la Kenya kesho atasaini
Mkataba wa kuichezea Simba katika msimu ujao.
Kiungo huyo
anayechezea klabu ya Afad Abidjan ya Ivory Coast amesema matarajio yake ni
kusaidia Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na hatimaye
kuwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa .
“Naijua
Simba ni timu kubwa lakini kwa hivi karibu haijawezza kushiriki mashindano ya
kimataifa hivyo nitacheza kuhakikisha timu inafanya vizuri ili kukata kiu ya
mashabiki”, alisema Kwizera
Mchezaji
huyo atakuwa wanne kwa wachezaji wa kigeni huku akisubiriwa Paul Kiongera kukamilisha
idadi ya wachezaji watano wa kigeni kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara.
Wachezaji wa kigeni waliopo Simba ni mabeki Mkenya Donald Mosoti, Mganda Joseph Owino na mshambuliaji Amisi Tambwe wa Burundi.
Wachezaji wa kigeni waliopo Simba ni mabeki Mkenya Donald Mosoti, Mganda Joseph Owino na mshambuliaji Amisi Tambwe wa Burundi.
No comments:
Post a Comment