Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, August 1, 2014

KITENDAGURO FC KUCHEZA FAINALI, WAICHAPA KAGONDO FC BAO 2-1 KAGASHEKI CUP.

TIMU ya Kitendaguro Fc Maarufu kwa jina la Makhirikhiri wameendelea na Makali yao tena leo baada ya kuifunga timu ya Kagondo Fc bao 2-1 na kusanga Fainali. Timu ya Kitendaguro waliwafunga juzi Rwamishenye kwa katika Mikwaju ya Penati mchezo ambao ulipigwa katika dakika 120 lakini leo mambo yalikuwa tofauti walishinda ndani ya dakika 90 tu.
Kitendaguro ndio walianza kuwafunga timu ya Kagondo mapema katika kipindi cha kwanza kwa Mkwaju wa penati katika ya dakika 10, mkwaju huo ulizamishwa na Hamis Itte. Kagondo Fc wao walipata bao la kusawazisha katika dakika ya 40 kupitia kwa Ditrick Stidius kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Kitendaguro Mbeki Ntambala.Kipindi cha pili Kitendagiro Fc waliongeza bao la Ushindi katika dakika ya 52, Bao likifungwa na mchezaji Nassoro Jumanne. Ushindi huu wa Kitendaguro unawapeleka Fainali na watakutana uso kwa Uso na Timu ya Miembeni Fc siku ya Jumapili kama ratiba inavyosema. Wao Kagondo Fc waliofungwa leo watachuana siku ya Jumamosi na waliokuwa mabingwa Watetezi wa Mashindano haya ya Kagasheki Bilele Fc siku ya Jumamosi kutafuta mshindi wa tatu bora. Mchezaji wa Kitendaguro Hamis Itte akimfunga kipa wa Kagondo Fc kwa mkwaju wa penati mapema dakika ya 10 na Kitendaguro kutangulia kwa bao 1-0 dhidi ya Kagondo Fc.Hamis Itte(kulia) wa Kitendaguro Fc akiwatoka wachezaji wa Kagondo Fc.Patashika kwenye lango la Kagondo Fc.Ilikuwa ni mshike mshike kila timu ikitaka kupata alama tatu muhimu na kwenda FainaliHamis Itte alionesha kiwango sana leoNani zaidi: Mchezai wa Kitendaguro Fc Fortunatus Shafick akikacha na mpira huku akikimbizwa vikali!Kagondo walifanya shambulizi na kuweza kusawazisha bao katika dakika ya 40 kipindi cha kwanza kwa shuti kali la Ditrick Stidius na kufanya 1-1Wachezaji wa Kagondo wakifurahia goli lao la kusawazishaNao Kitendaguro walipongezana baada ya kupata bao la pili na kufanya 2-1 Mtanange ulipomalizika katika dakika 90 wachezaji wa Kagondo Fc walikuwa na jaziba sana huku wakiwatupia maneno Waamuzi wa mtanange huo wa leoLakini Waaamuzi waliwaacha na kusonga mbele kwenda kwenye Vyumba vyao vya kupumzikia katika Uwanja wa Kaitaba.

No comments:

Post a Comment