Didier
Drogba amerejea tena Chelsea kama mpya na huenda akacheza mchezo wa Jumatano
|
Didier
Drogba amerejea tena kama kinda wa Chelsea kufuatia kuanza
mazoezi na kikosi cha timu kabla ya kuanza kampeni ya kuwania taji msimu
mpya.
Raia
huyo wa Ivory Coast alikamisha taratibu za kurejea Stamford Bridge wiki iliyopita
baada ya kuwa nje ya kikosi hicho kwa miaka na leo akianza mazoezi kwa
mara ya kwanza na wenzake katika uwanja w mazoezi wa Papendallaan huko
Arnhem nchini Uholanzi.
Licha
ya wachezaji aliokuwa nao hapo kabla kama Frank Lampard na Ashley Cole
hawako kikosini Drogba anaamini usajili uliofanywa na klabu hiyo msimu
huu wa kiangazi kama Fabregas,
Diego Costa na Filipe Luis kinaweza kujenga zama mpya kwa 'Blues'.
Mourinho na Drogba wakiwa pamoja tena kabla ya kuanza kampeni ya pamoja kuwania taji la Premier League baada ya miaka tisa kupita |
No comments:
Post a Comment