Waandaaji
wa mbio za Kilimanjaro Marathon wametangaza njia mpya zitakazotumika kwa mbio
za mwaka huu ikiwa ni hatua nyingine muhimu katika mafanikio ya mbio hizo
ambazo sasa zinaingia mwaka wa 12 tangu kuanzishwa.
Njia mpya
zimelenga kuboresha mwendo wa washiriki barabarani na kuwafanya wafurahie zaidi
mbio hizo zilizopangwa kufanyika tarehe 2 Machi, 2014 mjini Moshi.
Akitangaza
njia hizo mpya jana, John Addison, Mkurugenzi wa Wild Frontiers, waandaaji wa
mbio hizo alisema alisema: Tumeanzisha njia mpya ili kuzuia msongamano wa watu
wakati wa mbio kutokana na kuongezeka idadi ya washiriki kila mwaka.
Washiriki
wa mbio ndefu za marathon ya km 42, nusu marathon km 21, mbio ya walemavu na
mbio ya kujifurahisha ya Vodacom 5km Fun Run sasa hawatapishana tena barabarani
bali kila njia itatiririka katika muelekeo mmoja.
“Pia
kutokana na mabadiliko haya washiriki watakuwa wameepuka kilomita 3 za mwinuko
mkali kuelekea Chuo cha Mweka ambapo awali ndio palikuwa mahali pa kugeuzia
washiriki wa mbio za full marathon na nusu marathon. Mbio ya walemavu za Gapco
ambazo zitakuwa na makundi mawili tu mwaka huu ya kiti cha magurudumu
(wheelchair) na baisikeli ya mikono (handcycle) imefupishwa kutoka nusu
marathon na kuwa kilomita 10 ili kutoa fursa kwa watu wengi zaidi kushiriki na
njia sasa itapita eneo tambarare na lenye kivuli.
Mbio ndefu
za Kilimanjaro Premium Lager 42km Marathon zitaanza saa 12.30 asubuhi kutokea
uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara (MUCCoBS) na kuelekea barabara
iendayo Dar es salaam kwa kilomita kumi na kurudia geti la ushirika halafu
zitaenda kilomita 8 kuelekea hospitali ya KCMC na kukata kushoto hadi Barabara
ya Lema (Lema Road).
Wanariadha
watatelemka na Lema Road wakitelemka kupitia shule ya ISM halafu watamalizia na
kipande tambarare cha Barabara ya Kilimanjaro na kipande cha mita chache za
barabara ya Sokoine kuelekea uwanjani.
Mbio za
Nusu Marathon zitaanza saa moja kamili asubuhi kutokea MUCCoBS na kupandisha
kaskazini kuelekea hospitali ya KCMC kwa kilomita 8 ambazo ni sawa na ongezeko
la mwinuko wa futi 250 kutoka usawa wa bahari. Halafu mbio hizo pia zitapita
njia ya Lema Road na kurudi uwanjani.
Addison
alisema kuwa mbio za full marathon na nusu marathon zinapita kwenye maeneo
mbalimbali yenye vivutio na mandhari nzuri ya mji wa Moshi na sehemu zenye
mandhari ya mashamba ya kahawa na migomba jambo ambalo pia litawavutia wananchi
wengi kujitokeza kuwashangilia wanariadha.
“Njia zote
zitakuwa na vituo vya maji vya kutosha ili kuwafanya wanariadha wafurahie mbio
bila kushikwa na kiu muda wote wa mbio. Vilevile, njia nzima itakuwa na
madaktari na wauguzi wa kutoa huduma ya kwanza pamoja na magari ya kutosha ya
wagonjwa huku mamlaka husika zikidhibiti usalama wa wanariadha barabarani.
Madaktari
wengine na wauguzi wataukuwa uwanjani ambapo kutakuwa na zahanati ya dharula
kwa ajili ya huduma ya kwanza na kuchua misuli.
Mbio ya
walemavu ya Gapco Disabled 10km Marathon itaanzia uwanja wa MUCCoBS na kufata
barabara ya Kilimanjaro halafu mpaka Lema Road na kugeuza.
Addison
alisema mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run zitaanzia kwenye mzunguko
wa YMCA upande wa barabara ya Arusha na zitaenda hadi kwenye mnara wa saa
halafu kupita Boma Road kuelekea mzunguko (roundabout) wa barabara ya
Arusha na mzunguko wa YMCA tena na watapita Uru Road na kuingia uwanjani
kupitia geti la mashariki.
Executive
Solutions ni waratibu wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2014 wakishirikiana na
Riadha Tanzania, Chama cha Riadha Kilimanjaro na Kilimanjaro Marathon Club huku
zikidhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager (wadhamini wakuu), Vodacom Tanzania,
GAPCO, Simba Cement, and KK Security among others, Keys Hotel, TPC Sugar,
TanzaniteOne, CMC Automobiles Ltd, RwandAir, FNB Tanzania, UNFPA na Kilimanjaro
Water.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment