WINGA machachari wa Polisi Dar es Salaam
inayocheza Ligi daraja la kwanza Tanzania Bara, Hamis Mroki amefuzu majaribio
nchini Thailand kwenye timu ya Kabin United.
Mroki ambaye amewahi kuchezea Mtibwa na
timu za Taifa za vijana Serengeti boys
na Ngorongoro heroes ‘U-23’ amefuzu kuchezea timu hiyo ya daraja la pili baada
ya kufanya majaribio kwa siku mbili badala ya siku 30 kama walivyokubaliana na
timu hiyo.
Pia anasema kocha wa timu hiyo alivutiwa
naye baada kuona ana uwezo wa kucheza nafasi nyingi kitu ambacho ni nadra kwa
wachezaji wengi.
“Nilikuwa nifanye majaribio kwa siku 30
lakini nashukuru baada ya siku mbili nilifuzu kutokana na kiwango changu
kumridhisha kocha na sasa ndio nafuatilia Uhamisho wa Kimataifa hapa TFF ili
niondoke”, alisema Mroki
Mroki anacheza namba 7, 8, 11 na wakati
mwingine namba 10 kutokana na mfumo wa timu utakaokuwa unacheza.
Pia alisema Polisi Dar imekubali aondoke
kwani awali walikubaliana akipata timu nje ya nchi watamruhusu kuondoka na
amelishukuru Shirikisho la Soka Tanzania kwa kumpatia ICT ili aweze kuendeleza
kipaji chake.
No comments:
Post a Comment