Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linazitakia kila la kheri klabu za Yanga na
Azam ambazo timu zake zinatuwakilisha kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa
Afrika (CL) na Kombe la Shirikisho (CC).
Yanga
inacheza na Komorozine ya Comoro katika mechi ya kwanza ya raundi ya awali ya
CL itakayochezwa leo Februari 8 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
kuanzia saa 10 kamili jioni.
Nayo
Azam inaikaribisha Ferroviario de Beira ya Msumbiji katika mchezo wa kwanza wa
raundi ya awali ya CC utakaochezwa Jumapili Februari 9 mwaka huu saa 10
kamili kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.
Ni
matumaini yetu kuwa timu hizo mbili zitatuwakilisha vizuri kwenye michuano hiyo,
na kuwataka Watanzania wajitokeze kwa wingi viwanjani kuziunga mkono hasa kwa
vile zinacheza nyumbani.
No comments:
Post a Comment