Gervinho,
Juzi Jumatano, alifunga Bao 2 na kuipa ushindi AS Roma wa Bao 3-2
walipocheza na Napoli kwenye Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya Coppa
Italia na Curva Sud, eneo la Stadio Olimpico wanaloketi Kundi la
Mashabiki machachari waitwao Ultras kuibuka na kushangilia kwa kuimba:
‘Gervinho!’
Kwa Ultras kumsifia Mchezaji, hasa Mweusi, ni kitu adimu na hii imedhihirisha kuwa Gervinho, baada Miezi 6 kuwa na AS Roma ya Italy, kufuatia Miaka miwili akiwa huko London na Klabu ya Arsenal na kuonekana ‘bomu’, sasa ni moto.
Baada ya Mechi hiyo, anga zote za huko za Italy, za Wachambuzi wa Soka, zilijaa sifa za Straika huyo kutoka Ivory Coast aliihama Arsenal mwanzoni mwa Msimu kwenda AS Roma.
Kawaida Mchezaji akibadili Timu huibuka upya lakini mwenyewe Gervinho amedai kuungana tena na Kocha kutoka Ufaransa, Rudi Garcia, ambae walikuwa nae kwenye Klabu ya Lille huko Ufaransa, ndio kumemsaidia sana.
Amesema: “Tofauti kubwa kati ya Roma na Arsenal ni Kocha. Kocha wangu hapa, Garcia, amerudisha imani yangu. Kwa sababu ananiamini. Nikiamka Asubuhi nafurahia kwenda Kazini. Nafurahia kukutana na Wachezaji wenzangu!”
Hata hivyo, Gervinho hakuficha na kutofurahishwa na wakati wake huko Arsenal.
Akiwa na Goli 8 na AS Roma, zikiwemo 4 katika Mechi 3 zilizopita, amezungumza kuhusu Arsenal: “Nini nimejifunza huko Arsenal? Sikupata lolote kwa sababu muda wote niko Benchi tu. Nimeondoka huko kwa sababu nilikuwa sichezi!”
Nae kocha wa AS Roma, Rudi Garcia, amezungumza: “Ana kipaji. Anaweza kutoka nyuma, kuhadaa Wapinzani kwa spidi kali. Hatabiriki kwa Mabeki. Gervinho ni aina ya Mchezaji ambae lazima umpe imani ili acheze vizuri!”
Vile vile Garcia alikiri kuwa, kwa sababu ya historia yao tangu huko Lille, yeye hampendelei Gervinho na huwa mkali kwake na hilo limemfanya awe bora.
Nahodha wa AS Roma, Francesco Totti, ametoboa kuwa mafanikio ya AS Roma hivi sasa ni kwa sababu ya Gervinho.
Hivi sasa AS Roma wako Nafasi ya Pili kwenye Serie A.Gervinho akipongezwa na wenzake wa As RomaTwnzetu Bosi...Rudi Garcia na Gervinho
No comments:
Post a Comment