BONANZA LA MICHEZO LA JAMBO BUKOBA LAFANA
Mageni
Rasmi alikuwa ni Mheshimiwa mkuu wa mkoa kanali mstaafu Fabian Inyasi
Massawe(kulia) na hapa alikuwa anateta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba
Mheshimiwa Zipporah Pangani. Baada ya Bonanza hilo kufunguliwa Rasmi na
Mkuu wa Mkoa wa Kagera.Na Faustine Ruta, Bukoba.
Bonanza hili Lilianza kwa Maandamano(Marching to Kaitaba Stadium) ambapo ndipo Bonanza hilo limefanyikia tangu Asubuhi mpaka mchana. Bonanza hili pia lilishirikisha Shule mbalimbali za hapa Mkoani Kagera. Ambapo wanafunzi hao wamefanya maonesho mbalimbali kama, Ngoma, Michezo ya Bonanza, Sarakasi(Gymnastics) Mpira wa Miguu wasichana kwa wavulana. Pia kulikuwa na Kikundi cha Kakau Band cha hapa Bukoba. Zawadi na Vyeti vimetolewa kwa washindi. kumbuka Jambo Bukoba is a charitable organization which supports children and young people (mainly between the age of 5 and 19) in the field of healthcare (HIV), equality (equal rights) for girls , education and sports.
Mageni
Rasmi alikuwa ni Mheshimiwa mkuu wa mkoa kanali mstaafu Fabian Inyasi
Massawe (kulia) akiteta na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mheshimiwa Zipporah
PanganiTaswira
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Karwoshe wakiingia kutumbuiza kwa Ngoma
Kulia
ni Mr. Clemens Ndyetabura Mulokozi, Mwanzilishi wa Taasisi ya Jambo
Bukoba,Anayefata ni Mr. Gonza wakifurahia ngoma hiyo ya Utamaduni kutoka
kwa wanafunzi hao wa Shule ya Karwoshe
Furaha ikakolea!!
Mr. Clemens Mulokozi na Mr. Gonza....mambo safi
Kakau Band Bukoba wanasifika kwa kuachia Burudani hapa Bukoba na kwingineko..
Kakau Band wakinyonga nyonga muziki wao na kuwapa burudani wadau wao!
Kutoa Burudani...ni kazi yetu ...acha tufanye!!
Wana Kakau Band wakendelea kufanya kilichowaleta uwanjaniPongezi hapa!
Mzungu akishuhudia Mzungu mwenzake akijiachia na Ngoma ya Kibukoba ...Kakau!!
Tuanze jamani msiniache kistep!
Nimeweza au??? Mzungu wa Ugerumani akiiga kucheza ngoma na wana Kakau Uwanjani Kaitaba.
Ikawa ni full kujichanganya!!!
Post a Comment