TIMU
ya Yanga imeonesha matunda ya kambi yake iliyopiga Uturuki baada ya kuanza
vizuri mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania bara kwa kuibuka na ushindi wa
mabao 2-1 dhidi ya Ashanti United, mchezo uliopigwa dimba la taifa jijini Dar
es Salaam.
Mabao ya Yanga yalifungwa
na Didier Kavumbagu katika dakika ya 61 na David Luhende katika dakika ya 80.
Katika mchezo huo, kipindi
cha kwanza timu zote zilikosa nafasi nyingi za wazi za kufunga, huku Yanga
ikipoteza nafasi tatu kupitia kwa Kavumbagu, Said Bahanuzi na Mrisho Ngassa.
Kwani Kavumbagu alibaki
yeye na kipa na akataka kumpiga chenga, lakini kipa, Daudi Mwasonge aliweza
kuokoa hatari hiyo.
Nao Ashanti walionekana
kuchangamka, huku mchezaji wake, Bright Obinna akipoteza nafasi ya wazi ya
kufunga baada ya kumpiga chenga, Juma Abdul beki wa kulia wa Yanga.
Dakika ya 37 Yanga ilimtoa
Bahanuzi na nafasi yake kuchukuliwa na Saimon Msuva na Haruna Niyonzima alikosa
nafasi ya wazi ya kufunga eneo la hatari baada ya shuti kale kupaa.
Dakika ya 44, Husen Sued wa
Ashanti alikosa nafasi ya wazi kutokana na uimara wa kipa wa Yanga. Kwa ujumla
kipindi cha kwanza timu zote zilitoshana nguvu.
Kipindi cha pili Yanga
walikianza kwa kasi na walifanikiwa kupata bao la kwanza katika dakika ya 52
likifungwa na Kavumbagu akiunganisha pasi ya Simon Msuva.
Mara baada ya kuingia kwa
bao hilo, Ashanti walijitahidi kulishambulia lango la Yanga na wakapata bao la
kusawazisha dakika ya 61 likifungwa na Obinna aliyemalizia kazi nzuri ya Hussen
Sued.
Wakati mchezo huo
ukitazamiwa kumalizika kwa sare ya bao 1-1, David Luhende akaifunga Yanga bao
la pili katika dakika ya 80 na kuihakikishia pointi zote tatu.
Kwa matokeo hayo sasa Yanga
inaendelea kuongoza msimamo wa Ligi kuu kwa kujikusanyia pointi 31 baada ya
kushuka dimbani mara 14.
Kikosi cha Yanga kilikuwa;
Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Kevin Yondan, Frank
Domayo, Mrisho Ngassa, Haruna Niyonzima, Didier Kavumbangu/Hussein Javu, Said
Bahanuzi/Simon Msuva na David Luhende.
Ashanti United; Daudi
Mwasongwe, Hussein Mkongo, Abdul Mtiro, Shaffi Hassan, Tumba Swedi, Mohammed
Fakhi, Abdul Manani/Iddi Suleiman, Fakih Hakika, Bright Obinna/Paul Maona,
Hussein Swedi na Joseph Mahundi na Deogratias Munish "Dida".
NAMUNGO FC YAICHAPA COASTAL UNION 1-0 RUANGWA
-
TIMU ya Namungo FC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union
katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa
Majaliwa, Rua...
NMB YAZINDUA TEKNOLOJIA MPYA YA KISASA NA SALAMA
-
BENKI ya NMB imedhihirisha kiwango cha juu cha ubunifu, baada ya kuwa ya
kwanza nchini kuzindua Teknolojia Mpya, ya Kisasa na Salama Zaidi ya Mfumo
wa M...
Tarangire in a Heartbeat!
-
Big thanks to *Divine Eneja and Milou* for choosing Mobila Safaris for
their epic Tarangire day trip!
From the giant Baobabs to the massive ...
Post a Comment