Kenya imekosolewa na Shirika la kudhibiti matumizi ya
dawa za kusisimua misuli kwa kukosa kufanya uchunguzi katika ongezeko
la visa vya wakimbiaji wa Kenya wanaoshukiwa kutumia dawa hizo.
Tangu mwaka wa 2012 wakimbiaji 17 wamesimamishwa
kwa muda kutoshiriki mashindano ya kimataifa kwa madai ya utumizi wa
dawa hizo za kusisimua misuli, ikilinganishwa na 2 tu kati ya mwaka wa
2010 na 2011.
Shutma hizi zitazungumziwa katika
kongamano la shirikisho la kukabiliana na matumizi ya matumizi ya dawa
za kusisimua misuli katika michezo huko Johannesburg mwezi ujao
Ingawa shirika hilo halina uwezo wowote wa kuiwekea Kenya vikwazo, linaweza kuamua kuwa Kenya haifuati Sheria iliowekwa.
Hata hivyo ni jukumu la baraza la kimataifa la
michezo ya Olimpiki kuamua ikiwa wachezaji wanaweza kusimamishwa
kukimbia siku zijazo.
"Ikilinganishwa na nchi zingine, tatizo la Kenya si kubwa zaidi" amesema mwenyekiti wa wanariadha wa Kenya, Isaiah Kiplagat.
Vikwazo hizo zinaonekana kutotekelezwa kwa sasa,
lakini mkurugenzi wa shirikisho la kukabiliana na matumizi ya dawa za
kusisimua misuli David Howman ameuudhika kwa sababu Kenya haijachukua
hatua zozotete tangu madai hayo kutolewa.
David anatarajiwa kutaja Kenya kama nchi ngumu kushirikiana na shirikisho lake katika kongamano hilo huko Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa wanariadha wa Kenya
Isaiah Kiplagat na wizara ya michezo, shirikisho la kukabiliana na
matumizi ya dawa ya kusisimua misuli iliwapa fursa hadi Novemba mwaka
huu kutoa ripoti kuhusu hatua walizochukua lakini BBC imebaini kuwa,
chini ya wiki mbili kabla ya kongamano hilo, hamna habari zozote kutoka
kwa chama cha wanariadha cha Kenya.
Imebainika kuwa baraza lililoundwa na mashirika
ya michezo ili kuangazia madai hayo kwa haraka, halijawahi kufanya
mkutano tangu kuundwa mwaka uliopita.
Rodney Swigelaar mkerugenzi wa shirikisho la kukabiliana na dawa za kusisimua misuli barani Afrika alisema:
"Tumekufa moyo, ni zaidi ya mwaka mmoja sasa tangu twende huko na hata zaidi tangu uvumi wa madai hayo kuanza.
"hatua yao ya kuakhirisha uchunguzi imetuudhi,siwezi kusema rasmi wamefikisha wapi upelezi wao.
"Tumekua watulivu sana, wakati mambo haya
yanafanyika mahali popote, ni jukumu letu kwenda kule na kuuliza ni nini
chanzo chake na ni kwanini watu hawafuati sheria"
Lakini Kiplagat ameiambia BBC
"naweza
kudhibitishia kila mmoja kuwa baraza lililobuniwa na serikali itaanza
kazi yake hivi karibuni.
Tunatumai upelezi huo utaanza kabla ya kongamano
la shirikisho la (WADA) kuanza. Sidhani matumizi ya dawa hizo ni tatizo
kubwa sana Kenya. Wanariadha wetu wakuu walipimwa kabla ya kuenda London
na pia kabla ya mashindano ya kimataifa ya IAAF huko Moscow mwaka huu.
Hata hivyo WADA inaweza kubuni kamati huru nchini Kenya kama ilivyofanya Jamaica licha ya uhakikisho wa Kiplagat.
No comments:
Post a Comment