Arsenal wamewasha moto, ushindi wa jumanne dhidi ya napoli ni ushindi wao wa 10 mfululizo msimu huu.
Mabao ya kipindi cha kwanza ya mesut ozil na olivier
giroud, yamewafanya vijana wa arsene wenger kukaa kileleni mwa kundi f, miamba
hiyo ya emirates iko kileleni mwa msimamo wa ligi kuu england kutokana na
kushinda mechi tano kati ya sita msimu huu.
Hizi ndizo siri 10 za mafanikio ya arsenal msimu
huu.
Giroud
mtambo wa mabao
Siyo tu kwamba, olivier giroud amenyoa staili mpya,
sasa hivi anaweza kujifagilia kwamba ni mmoja kati ya washambuliaji bora
england. Mfaransa huyo anaongoza mashambulizi ya arsenal kwa mifano, tayari
anamabao sita msimu huu.
Wenger alitaka kusajili straika mpya, wakati wa
kiangazi alitoa ofa kwa gonzalo higuain, luis suarez na wayne rooney na
kushindwa kwake kuwanasa kulitoa dalili za ukame kuendelea arsenal, lakini
giroud anamtazamo mwingine na kazi yake ni moja tu kucheka na nyavu.
Flamini
amerudi kukichafua
Mathieu flamini (28), alirudi rasmi emirates kwa
mara ya pili kwenye mechi dhidi ya tottenham hotspur. Aliingia kipindi cha pili
kwenye mechi hiyo na kukichafua kwenye eneo la kiungo na kusababisha viungo wa
timu pinzani kupaona pachungu na tangu wakati huo jamaa kazi yake ni moja tu,
kutibua.
Kwa kipindi kirefu sasa, arsenal wamekosa kiongozi
kwenye kikosi chao na flamini anaweza kuwa jibu lao. Jamaa amekuwa akitawala
kiungo cha arsenal na kufanya maisha kuwa magumu kwa wapinzani kutokana na
ubabe wake na buti zake za chini chini ambazo zimekosekana arsenal kwa muda
mwingi.
Mwaka 2008 aliondoka arsenal na kukimbilia ac milan
kutafuta mafanikio, lakini sasa hivi amerudi akiamini bado anadeni kwa arsene
wenger na anaonekana kulipa kila kitu kwa sasa.
Wenger alimfagilia sana ozil baada ya arsenal kuipiga
napoli, lakini shughuli aliyoifanya flamini ilikuwa siyo mchezo na kuwapa
nafasi kina ozil, aaron ramsey na thomas rosicky kucheza huru.
Mchawi
ozil
Saa moja likiwa limesalia kabla ya dirisha la
usajili kufungwa, taarifa zilizagaa kwamba arsenal wamenasa mmoja kati ya
wachezaji bora duniani. Wenger anajulikana kwa ubahili wake, kwa mjerumani huyu
alivunja rekodi ya usajili ya klabu.
Mesut ozil ametua arsenal kutoka real madrid kwa ada
ya pauni milioni 42.5 na macho huyo wa kijerumani anaonekana kurudisha kila
shilingi iliyotumika kumsajili. Ozil ana kila kitu anajua kukaa na mpira,
fundi, mbunifu na ‘timing’.
Bao lake la kwanza kwenye jezi za arsenal katika
pambano dhidi ya napoli, lilikuwa la kuvutia sana na mashabiki wa arsenal sasa
wanaona fahari kuvaa jezi zao walizokuwa wamezifungia kabatini kutokana na
matokeo mabovu.
Nini
bale, kuna ramsey
Mchezaji wa kimataifa wa wales anayetajwa sana ni
gareth bale, lakini sasa hivi arsenal kuna aaron ramsey (22), moja ya wachezaji
ambao msimu uliopita alikuwa akichukiwa mno na mashabiki wa miamba hiyo ya
emirates, lakini sasa hivi ndiyo kila kitu kwao, amekuwa kipenzi chao kutokana
na fomu yake ya kufunga mabao muhimu msimu huu.
Ramsey tayari amefunga mabao manne kwenye ligi kuu
england, manne ligi ya mabingwa ulaya na moja akiwa na timu ya taifa ya wales.
Siyo mabao yake tu ndiyo yamechangia mafanikio ya
arsenal msimu huu, lakini pia kujituma kwake kumekuwa hakuna mfano, anahaha
uwanjani msimu, jina lake sasa hivi ndiyo la kwanza kuandikwa kwenye karatasi ya
kikosi cha wenger akiwa anapanga timu, sasa hivi london kuna mchawi mpya wa
wales na tumpotezee bale.
Nyumbani
ni nyumbani
Emirates hapajawa nyumba yenye furaha arsenal tangu
walipoondoka highbury mwaka 2006, lakini kwa jinsi hali ilivyokuwa emirates
jumanne usiku, ni wazi sasa hali inabadilika.
Mashabiki wa arsenal waliokuwa wakigombana juu ya
mustakabali wa wenger na utawala wa arsenal, waliungana na kuwa kitu kimoja na
kuishangilia timu na wachezaji, wanaonekana kutambua sapoti ya mashabiki.
Ukuta
wa berlin umekamilika
Siku za nyuma beki ya arsenal ilikuwa kichekesho
england, lakini sasa hivi ukuta wa berlin umejengwa upya arsenal. Laurent koscielny
anausoma mchezo kama kitabu, wakati per mertesacker anaonyesha kwanini amecheza
mechi karibu 100, ujerumani. Bacary sagna na kieran gibbs wamemaliza matatizo
yao ya majeruhi.
Vipi kuhusu wojciech szczesny? Siku zote amekuwa
akijiamini, lakini sasa hivi anathibitisha ubora wake.
Kikosi
kikubwa
Neno hili ni geni kwa arsenal. Lakini baada ya ujio
wa ozil na flamini, wenger amefanikiwa kuwa na wachezaji lukuki wa kuchagua
kati kati ya uwanja.
Jack wilshere alianzia benchi jumanne usiku, huku
theo walcott, alex oxlade-chamberlain, santi cazorla na lukas podolski
hawakuwepo kabisa. Na hutakiwi kumsahau abou diaby. Swali je, wenger atawafanya
mastaa wote wawe na furaha?
Kucheza
kitimu
Mafanikio uwanjani yanatokana na kujiamini na umoja
wa wachezaji. Umoja ni kitu ambacho kinaonekana sasa hivi arsenal ikiwa pamoja
na kucheza kitimu.
Utani kwenye viwanja vya mazoezi, kupeana tano baada
ya bao kufungwa na picha za kushangilia bao zikiwekwa kwenye mitandao ya
kijamii baada ya mechi, hakuna ubishi kwamba vijana wa london kaskazini wanafuraha
na umoja.
Mwanzo
mzuri
Wakati manchester united wakianza kwa ratiba ngumu
sana, arsenal wamekuwa na mwanzo rahisi, ukitoa mechi za tottenahm na napoli tu,
ambao wote wamekutana nao nyumbani na the gunners wasingeweza kuwa na ratiba
rahisi zaidi ya hii. Kazi inakuja kwa mechi dhidi ya chelsea, liverpool na
borussia dortmund ambazo ziko njiani.
Wenger
‘the boss’
Siku hizi mashabiki wa arsenal hawaimbi sana jina
lake kama zamani, lakini kiitikio cha wimbo wa there's only one arsene wenger,
jumanne usiku kilisikika kwenye paa la emirates mashabiki waliimba kwa
kumfagilia kocha wao.
Mfaransa huyo almanusura apoteze kibarua chake baada
ya kichapo cha aston villa katika mechi ya ufunguzi wa ligi, lakini aligoma
kukurupuka na kumsajili flamini bure na ozil. Swali ni je, huu ni mwaka wake wa
kumaliza ukame wa miaka nane bila taji?
No comments:
Post a Comment