Pambano
la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Azam lililochezwa jana (Oktoba
28 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 64,261,000.
Washabiki
waliohudhuria mechi hiyo namba 76 iliyomalizika kwa Azam kuibuka na
ushindi wa mabao 2-1 walikuwa 10,728 ambapo viingilio vilikuwa sh.
5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Mgawo
wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) sh. 9,802,525.42, gharama za kuchapa tiketi sh. 3,793,490 wakati
kila klabu ilipata sh. 14,946,170.45.
Wamiliki
wa uwanja walipata sh. 7,599,747.49, gharama za mchezo sh.
4,599,848.61, Bodi ya Ligi sh. 4,599,848.61, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira
wa Miguu (FDF) sh. 2,279,924.31, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar
es Salaam (DRFA) sh. 1,773,274.46.
No comments:
Post a Comment