Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, October 3, 2013

ISRAEL NKONGO, LESLEY LIUNDA NA SOUD ABDI KUHUDHURIA KOZI YA FUTURO ADDIS ABABA

Mwamuzi Israel Nkongo (wa tatu toka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja katika moja ya mechi alizowahi kuchezesha

Watanzania watatu ni miongoni mwa washiriki 30 walioteuliwa kuhudhuria kozi ya wakufunzi ya waamuzi ya FUTURO III itakayofanyika Addis Ababa, Ethiopia kuanzia Oktoba 5 hadi 10 mwaka huu.

Leslie Leonard Liunda, Abdi Soud Mohamed na Israel Nkongo Mujuni ndiyo watakaoshiriki katika kozi hiyo itakayoendeshwa na wakufunzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Kozi hiyo pia itakuwa na washiriki kutoka nchi nyingine tisa za Afrika. Nchi hizo ni Gambia, Ghana, Kenya, Liberia, Nigeria, Seychelles, Sierra Leone, Somalia na Uganda.

No comments:

Post a Comment