Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, October 3, 2013

NIYONZIMA AUNGULIWA NA NYUMBA JIJINI DAR ES SALAAM LEO,, WASAMARIA WAOKOA FAMILIA YAKE



Kiungo nyota wa Yanga, Haruna Niyonzima ameunguliwa na nyumba yake anayoishi jijini Dar es Salaam.

Nyumba anayoishi ipo Magomeni jijini Dar es Salaam na moto huo ulianza saa 12 alfajiri hadi ulipozimwa na majirani saa moja asubuhi leo.



Taarifa zinasema nyumba hiyo imeungua kutokana na hitilafu ya umeme katika moja ya nyaya ndani ya nyumba hiyo.
Vitu kadhaa vya thamani vimeteketea kwa moto lakini familia yake imesalimika baada ya majirani kuwaokoa.



“Kweli ninawashukuru sana majirani kwa kuonyesha uungwana wa hali ya juu, bila ya wao nyumba yote ingeungua.

“Lakini kuna vitu vichache vimefanikiwa kutoka ila vingi sana vimeungua na moto huo uliokuwa mkali sana,” alisema.
Hadi blogu hii inaondoka eneo la tukio asubuhi hii, baadhi ya watu na mashabiki wa Yanga walikuwa wamefika kwa ajili ya kutoa msaada zaidi.
Pia fundi wa umeme alikuwa anasubiriwa ili kuangalia hitilafu iliyosababisha moto ilitokana na kitu gani.
Kwa hisani ya Salehjembe blog

No comments:

Post a Comment