Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, August 20, 2013

TAMASHA LA KILI MUSIC TOUR 2013 JIJINI MWANZA LILIVYOFANA

Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya (Bongo Fleva),Nassib Abdul a.k.a Diamond akiwajibika jukwaani sambamba na madansa wake wakati wa Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki na kuhudhuliwa na maelfu ya wakazi wa Mwanza na mikoa ya Jirani waliokataa kupitwa na Onyesho hilo kabambe.

Diamond akiwa amenyanyuliwa juu na madansa wake wakati wa Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki na kuhudhuliwa na maelfu ya wakazi wa Mwanza


Mkali wa Ryms afahamikae kama Joseph Haule au ukipenda waweza muita Profesa Jay wa Mitulinga akiwapagawisha vilivyo wakazi wa Jiji la Mwanza waliofurika kwa wingi ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba kwenye Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki na kuhudhuliwa na maelfu ya wakazi wa Mwanza


Wanamuziki wakongwe katika medani ya muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydee na Joseph Haule au ukipenda waweza muita Profesa Jay wakiburudisha maelfu ya mashabiki wa muziki waliofurika katika Uiwanja wa Ushirika mjini Moshi mwishoni mwa wiki katika muendelezo wa Maonyesho ya Tamasha la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013.

Mwanadada nguli katika tasnia ya Muziki hapa nchini, Muite Bint Komando au Lady Jaydee akifanya vitu vyake ndani ya jukwaa moja la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.

Wakongwe katika medani ya muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydee na Joseph Haule a.k.a Profesa Jay wakionyesha uhodari wao kwa kulishambulia jukwaa mbele ya maelfu ya mashabiki wa muziki waliofurika kwa wingi katika Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. 

No comments:

Post a Comment