TIMU ya Young Coaches jana iliifunga New Eleven bao 1-0 kwenye mchezo wa kombe la ng’ombe uliochezwa Uwanja
w Beira Msimbazi, Ilala
Mchezo huo ambao ulisheheni
wachezaji wa zamani ambao ndio wanaounda timu ya Young Coaches ulihudhuriwa na
umati mkubwa.
Young Coaches walijipatia
bao dakika ya 27 kupitia kwa mshambuliaji wao wa Kimataifa wa Nigeria George
Anyanwu baada ya kuunganisha pasi ya Shafii Dauda.
Kipindi cha pili kilianza
kwa timu zote kufanya mabadiliko hata hivyomabadiliko hayo hayakuweza
kubadilisha matokeo ya kipindi cha kwanza.
Akizungumza baada ya mchezo,
nahodha wa Young Coaches, Mohamed Husein “mmachinga” alisema kuwa mchezo
ulikuwa mzuri ila timu yao haina mazoezi ya kutosha zaidi uzoefu ndio
unawasaidia wasifungwe.
“Timu yetu hatuna mazoezi ya
pamoja ndio maana tunashindwa kufunga mabao mengi kwa sababu ya kukosa pumzi
ila uzoefu ndio unatubeba”, alisema Mohamed
Kikosi cha Young Coaches
kilikuwa na Moses Mkandawile, Shedrack Nsajigwa, Mwanamtwa Kihwelo, Athuman
Kipao, Zuberi Katwila, Shafii Dauda, George Anyanwu, Edibily Lunyamila, Emanuel
Gabriel, Shomari Chaurembo na Grayson Swai
Wengine ni Steven Nyenge,
Ally Yusufu ‘Tigana’, George Lucas, Zulfikri Idd, Collin Frich na Omari Mbarouk
No comments:
Post a Comment