WACHEZAJI wa timu ya Tiger ya mchezo wa Rollball huenda
wakashindwa kuhudhuria mafunzo kutokana ukata unaowakabili.
Timu hiyo imealikwa kushiriki mafunzo ya ukocha na urefa kwa
mchezo huo yatakayofanyika Nairobi
nchini Kenya kuanzia Julai 26 hadi Julai 29, mwaka huu.
Akizungumza jijini, Sylvester Kasembe ambaye ni mmoja wa
wachezaji wa timu hiyo alisema kuwa gharama za ushiriki kw mtu mmoja ni Ksh. 2500 ambazo ni sawa Tsh. 50,000 huku
gharama za nauli na malazi kwenda na kurudi ni Tsh. 200,000.
“Tunatakiwa kulipia ada ya ushiriki ambayo ni 50000 kwa mtu
mmoja pia nauli na malazi kwa siku zote ni 200000 hivyo mtu mmoja anatakiwa
kuwa na 250,000 hivyo watu 12 itakiwa
3,000,0000”, alisema Kasembe.
Kasembe amesema timu yao haina uwezo wa kuwasafirisha
wachezaji kuhudhuria mafunzo hayo hivyo wanaomba wadau wawasaidie ili waweze
kupata mafunzo hayo kwani ni sehemu ya maandalizi ya fainali za dunia
zitakazofanyika Otoba nchini Nairobi.
Rollball ni mchezo
unaochezwa kwa mikono kama mchezo wa
mikono (handball) huku wachezaji wao wakiwa wamevaa viatu vya matairi na kwa
sasa kiwanja cha mchezo huo kipo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Fainali za dunia za 2012 ambazo zilifanyika nchini India Tanzania
ilifika hatua ya robo fainali.
No comments:
Post a Comment