Mshambuliaji wa Sayari Fatuma Mustapha akiwatoka mabeki wa Vfl Kellinghusen ya Ujerumani wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam |
Mshambuliaji wa Sayari, Neema Kuga akiwatoka mabeki wa Kellinghusen |
Mwamuzi Rahel Pallangyo akiwakagua wachezaji wa Vfl Kellinghusen |
Sayari women |
Vfl Kellinghusen |
TIMU ya Sayari juzi iliifunga Vfl Kellinghusen ya Ujerumani mabao 9-1 kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam.
Sayari ambayo ilisheheni mamluki kibao ilikwenda mapumziko
wakiwa mbele kwa mabao 3-0. Yaliyofungwa na Fatuma Mustapha dakika ya 14 na 20
na Neema Kuga aliyefunga dakika ya 37.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko
lakini jahazi la Vfl Kellinghusen lilizidi kuzama baada ya kuongezwa mabao
mengine kupitia kwa Esther Chabruma dakika ya 58.
Mabao mengine ya Sayari yalifungwa na Sophia Mwasikili
alifunga mawili dakika za 61 na 86, Fatuma Mustapha tena alifunga bao dakika ya
75, Fatuma Bushiri dakika ya 85 msumari wa mwisho uligongewa na Sylvie Felix
dakika ya 89.
Timu ya Vfl Kellinghusen ilipata bao la kufutia machozi
kupitia kwa Jule Mohr dakika ya 52 lililotokana na mpira wa adhabu baada ya
beki wa Sayari Pulkeria Charaji kumfanyia madhambi mshambuliaji wa Vfl Kellinghusen , Annika Ehlers nje ya
eneo la hatari.
Akizungumza baada ya mchezo huo Katibu wa Chama
cha Soka la Wanawake mkoa wa Dar es Salaam, (DWFA) Stephania Kabumba alisema
anashukuru mchezo umechezwa vema na kuwapongeza Sayari kwa ushindi waliopata.
“Nashukuru mchezo umechezwa vema pia naipongeza Sayari kwa
ushindi waliopata kwani wamedhirisha kuwa soka la wanawake linaweza kupererusha
vema bendera ya nchi”, alisema Stephania.
No comments:
Post a Comment