Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, July 26, 2013

HUSEIN JAVU WA MTIBWA AANZA MAZOEZI YANGA

Klabu ya Young Africans imekamilisha usajili wa mshambuliaji Hussein Javu kutoka timu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani - Morogoro ambapo mchezaji huyo jana alianza mazoezi katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola Mabibo jijini Dar es salaam.

Hussein Javu amesajili Young Africans kwa mkataba wa miaka miwili ambapo atavaa jezi za watoto wa Jangwani mpaka mwishoni mwa msimu wa 2014/2015.Usajili wa Javu unafikisha idadi ya washambuliaji sita mpaka sasa wakiwemo Didier Kavumbagu, Jerson Tegete, Said Bahanuzi, Shaban Kondo (mpya - Msumbiji) na Realintus Lusajo (mpya kutoka Machava FC - Moshi).

Kikosi cha mholanzi Ernie Brandts kinaendelea na mazoezi kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom unaotarajiwa kuanza agosti 24 kwa kufungua dimba na timu ya Ashanti United iliyopanda msimu huu.

Agosti 17-2013  Young Africans itacheza mchezo wa Ngao ya Hisani na timu ya Azam FC katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu kwa msimu wa 2013/2014.

Mpaka sasa klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa wachezaji saba (7) wapya ambao ni:1. Deogratius Munishi 'Dida' -  Huru Azam FC (Golikipa)2.Rajab Zahir -  Huru Mtibwa Sugar  (Mlinzi wa kati)3.Hamis Thabit - Huru Ureno (Kiungo)4.Shaban Kondo - Huru Msumbuji (Mshambuliaji)5.Mrisho Ngassa - Huru Azam FC (Kiungo mshambuliaji)6.Reanlintus Lusajo - Huru Machava FC (mshambuliaji)7. Hussein Javu - Mtibwa Sugar (mshambuliaji)

Kikosi kinaendelea na mazoezi katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola kila siku saa 2 asubuhi na wachezaji waliopo katika timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) wanatarajiwa kuungana na wenzao katika mazoezi siku ya jumatatu.

No comments:

Post a Comment