Haendi kokote: Rais wa Real Madrid Florentino Perez akiwa na Cristiano Ronaldo.
Rais wa Real Madrid Florentino Perez amethibtisha kuwa mshambuliaji wake Critiano Ronaldo atamalizia kazi ya soka akiwa katika mji mkuu wa Hispania na kama inavyodhaniwa kwa sasa huenda akarejea United.
Kauli ya Rais huyo imeondoa shaka shaka iliyokuwepo hapo kabla ya kwamba Cristiano Ronaldo ataondoka katika klabu hiyo katika kipindi hiki cha kiangazi au kipindi kingine chochote cha uhamisho na hapo akikazia kuwa mreno huyo atamalizia soka yake katika mji mkuu wa Hispania Madrid.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno amekuwa akihusishwa na kurejea katika klabu yake ya zamani ya Manchester United au kujiunga na mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris St Germain.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 28 bado ana mkataba wa miaka miwili katika klabu hiyo ambayo ilimnunua kwa rekodi ya uhamisho ya dunia ya pauni milioni £80 kutoka United mwaka 2009.
Ronaldo akionekana pichani wakati wa mchezo wa jumapili baina ya Madrid na Bournemouth.
No comments:
Post a Comment