MACHANGUDOA BRAZIL WAANZA KUJIFUNZA KIINGEREZA
BELO HORIZONTE, Brazil
MACHANGUDOA nchini Brazil, wameanza kujifunza Kingereza ili
kutoa huduma motomto kwa maelfu ya mashabiki wa soka watakaoingia nchini humo
kwa ajili ya kushuhudia michuano ya Kombe la Mabara, Juni mwaka huu na ile ya
Kombe la Dunia mwakani.
Wasichana lukuki wanaofanya biashara ya kujiuza kwenye Jiji la
Belo Horizonte, wamekuwa wakihudhuria madarasa ya kingereza kwa ajili ya
kujifunza lugha hiyo.
Igor Fuchs amekuwa akifundisha machangudoa hao kingereza,
lakini amesema masoma hayo yanaangalia zaidi lugha za kimapenzi ili wasichana
hao wawe wajuzi wakati wakihudumia wateja kutoka mataifa mbalimbali.
Jiji hilo linamachangudoa zaidi ya 80,000, ambao wanasuburi
kwa hamu mashindano hayo, lakini uongozi wa Jiji hilo unategemea jumla ya
mashabiki 40,000 wataingia kwenye mji huo mwezi ujao, wakati zaidi ya mashabiki
140,000 watahudhuria fainali za Kombe la Dunia 2014.
Chama cha Machangudoa kwenye mji huo kimekuwa kikitoa elimu ya
bure ya somo la Kingereza kwa wasichana hao wanaojiuza tangu Machi mwaka huu.
“Tunawafundisha jinsi ya kujieleza, lakini pia tunawafundisha
kwa vitendo jinsi ya kutumia vifaa vya kufanyia mapenzi, iliwavijue kwa majina
na jinsi ya kuvitumia au kuomba kutumia.” Alisema Fuchs, ambaye anafundisha
lugha za Kihispaniola na Kifaransa pia.
Post a Comment