RONALDO OLD TRAFFORD


Hi-res-163463886_crop_north
MANCHESTER, England
JAVIER Hernandez ‘Chicharito’ atakuwa muhimu kwa mchakato wa Manchester United kumrudisha Cristiano Ronaldo, Old Trafford.

Man United walikuwa wamepanga kutoa kiasi cha pauni milioni 65 pamoja na Luis Nani kwa ajili ya kumnasa Ronaldo mwisho wa msimu huu, lakini Real Madrid wanamtaka Chicharito kwa pauni milioni 25 hata kama dili la usajili wa Ronaldo litakwama.

Paris Saint-Germain tayari wameshaweka mezani kiasi cha pauni milioni 80 kwa ajili ya Ronaldo — dau ambalo alisajili wa nalo alipotoka Man United mwaka 2009.

Mabingwa wa Ligi Kuu England, Man United ni moja kati ya klabu chache ambazo zinaweza kumsajili staa huyo wa Kireno mwenye miaka 28. Na juzi klabu hiyo ilitangaza kuingiza zaidi ya pauni milioni 92 kwenye miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 2013.

Chicharito anaweza kuwa muhimu sana kwenye kufanikisha usajili wa Ronaldo, ambaye mwenyewe anatamani sana kurudi Old Trafford, Japokuwa Sir Alex Ferguson anataka kumbakisha Mmexico Man United.

No comments