JUVENTUS YATEGA KWA ROBBEN

Juventus ipo tayari kutoa ofa kwa winga aliyeipa Bayern Munich Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Arjen Robben.

Licha ya kufunga bao la ushindi kwenye mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyopigwa katika Uwanja wa Wembley dhidi ya Borussia Dortmund, winga huyo wa zamani wa Real Madrid, hayupo katika mipango ya Kocha mpya, Pep Guardiola, imeelezwa katika TMW.

Lakini hiyo ni habari njema kwa Juve na Kocha wao, Antonio Conte, ambaye tayari ameanza kufukuzia sakata hilo.

No comments