Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, April 16, 2013

TAIFA STARS YAUNDIWA KAMATI YA USHINDI



SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo imeunda kamati maalumu kwa ajili ya kuisaidia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ili iweze kufanya vizuri kwenye michezo yake iliyobakia ya kufuzu michuano ya Kombe la dunia 2014. 

Hivi karibuni Stars ilifanikiwa kuifunga Morocco mabao 3-1 hivyo kufanikiwa kujiweka katika nafasi nzuri kwenye kundi C walilopo wakiwa na timu zingine za Ivory Coast na Gambia. Msimamo wa kundi hilo mpaka sasa Stars wako katika nafasi ya pili wakiwa na alama sita, nyuma ya vinara Ivory Coast wanaoongoza kwa alama saba na Morocco ni ya tatu wakiwa na alama mbili wakati Gambia wao wanashikilia mkia wakiwa na alama moja.

Kutokana na matokeo hayo wizara kupitia waziri wake Fenela Mukangara wameipongeza timu hiyo kwa kuweka matumaini hai ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Brazil 2014. na kwa kuzingatia hilo wizara imeamua kuunda kamati maalumu kwa ajili ya kuongeza hamasa ya ushindi kwa Stars ili iweze kuweka historia kwa kushiriki michuano ya Brazil. Jukumu la msingi la Kamati iliyoundwa ni kuhakikisha Taifa Stars inawezeshwa na kuandaliwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuunda kikundi cha kuishangilia timu ya Taifa ndani na nje ya nchi.

Wajumbe wa Kamati ya Taifa Stars Stars itakayoongozwa na Mhe. Mohamed Dewji ni hawa wafuatao:-


Mhe Mohamed Dewji - Mbunge
Bi. Teddy Mapunda - Montage
Dkt. Ramadhani Dau - Mkurugenzi Mtendaji NSSF
Bw. Dioniz Malinzi - Mwenyekiti BMT
Bw. Abji Shabir - New Africa Hotel
Bw. George Kavishe - TBL
Mhe. Mohamed Raza - Zanzibar
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Bw. Joseph Kusaga - Clouds
Mhe. Kapt. John Komba - Mbunge
Mhe. Zitto Kabwe - Mbunge

Kamati hiyo iliyoteuliwa leo, inatakiwa kuanza kazi kazi mara moja. Hadidu za rejea zitakazowaongoza kutekeleza majukumu yao chini ya Kamati hii watazipata kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kamati itashirikisha wadau mbalimbali kadri itakavyoona inafaa. Serikali inaahidi kutoa ushirikiano utakaohitajika katika kuhakikisha Kamati hii inafanya kazi vizuri ili kuiwezesha Taifa Stars kushinda Mechi zote zilizombele yetu.

No comments:

Post a Comment