Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la kwanza |
John David wa Azam na Haruna Chanongo wa Simba wakiwa wameangukiana |
Mshambulia wa Azam, Himid Mao akiondoka na mpira huku Haruna Chanongo akimwangalia |
John David wa Azam akiokoa mpira kwenye eneo la hatari huku Haruna Chanongo akifikiria jinsi ya kumnyanganya |
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao kwa staili ya aina yao |
Mwadini Ally akiwa amedaka mpira |
Kwa matokeo haya Azam imefikisha pointi 47, ikibaki nafasi
ya pili, nyuma ya Yanga yenye pointi 52, huku Simba ikibaki nafasi ya nne kwa
pointi zake 36.
Mabao ya Simba yalifungwa na Ramadhani Singano ‘Messi’
aliunganishia nyavuni mara zote mbili dakika ya 10 na 14 pasi za Mrisho Khalfan
Ngassa kutoka wingi ya kushoto.
Kipre Tchetche aliifungia Azam kwa penalti dakika ya 29,
baada ya Khamis Mcha kuangushwa kwenye eneo la hatari na William Lucian.
Mwamuzi Oden Mbaga
alimwondoa kwenye benchi kocha Muingereza wa Azam, Stewart Hall dakika ya 31
baada ya kulalamikia uchezeshaji wa refa huyo.
Kipindi cha pili, Azam walirejea kwa nguvu kusaka bao la
kusawazisha na wakafanikiwa dakika ya 72 baada ya Humphrey Mieno kuunganisha
shuti la mpira wa adhabu lililopigwa na kiungo Khamis Mcha.
Baada ya hapo, timu hizo zilianza kushambuliana kwa zamu na
mara kadhaa timu zote mbili zilikosa mabao.
Kikosi cha Simba SC
kilikuwa; Abbel Dhaira, Nassor Masoud ‘Chollo’, Miraj Adam, Mussa Mudde,
Shomari Kapombe, Amri Kiemba, Haroun Chanongo/Edward Christopher, Abdallah
Seseme, William Lucian/Mwinyi Kazimoto, Ramadhani Singano na Mrisho
Ngassa/Fliex Sunzu.
Azam FC; Mwadini Ally, Himid Mao, Waziri Salum, David
Mwantika, Joackins Atudo, Kipre Balou, Luckson Kakolaki/Khamis Mcha ‘Vialli’
dk, Salum Abubakar, John Bocco/Abdi Kassim, Humphrey Mieno/Jabir Aziz na Kipre
Tchetche.
No comments:
Post a Comment