Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, April 23, 2013

HUYU NDIE LUIS SUAREZ PATA UNDANI WAKE NA KISA CHA KUMNG'ATA IVANOVIC


LUIS SUAREZ (Liverpool)
Huyu ndiye Luis Suarez a.k.a ‘Mla watu wa Ajax’
*Tyson amkubali kwa kumpiga jino Ivanovic
* Alishawahi kumng’ata mtu akiwa Uholanzi

HILI ni tukio lililoushangaza ulimwengu wa soka juzi – baada ya Luis Suarez (26) akiwa na hasira kumng’ata beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic, katika pambano kati ya Liverpool na Chelsea lililomalizika kwa sare ya 2-2.
Tukio hilo la kushangaza lilitokea katika dakika ya 65 ya mchezo, kati ya timu hizo na kuwashtua mamilioni ya mashabiki waliokuwa wakitazama mechi hiyo na kuzua hasira huku wengi wakitaka afungiwe muda mrefu.
Hii ni mara ya pili kwa mshambuliaji huyo mtata kumng’ata mpinzani wake, aliwahi kufanya hivyo wakati akichezea klabu ya Ajax, mwaka 2010.
Kitendo ambacho kilimpa jina la utani la The Cannibal of Ajax (Mla Nyama za Watu wa Ajax) kutokana na kumng’ata begani kiungo wa PSV Eindhoven, Otman Bakkal — alifungiwa mechi saba kutokana na tukio hilo.
Usiku wa juzi mshambuliaji huyo wa Uruguay – ambaye amekuwa akitawaliwa na matukio ya utata – alikiri kumng’ata Ivanovic na kuomba radhi.
Suarez aliomba msamaha wake wa kwanza kupitia akaunti yake ya Twitter “Ni tabia isiyo vumiliika, nimesikitishwa na kilichotokea.”
Dakika chache baadaye aliomba radhi kupitia taarifa iliyotolewa na Liverpool, akisema amejaribu kumtafuta Ivanovic azungumze naye.
Suarez aliongeza: “Ninamuomba radhi pia kocha wangu, wachezaji na kila mtu kwenye klabu ya Liverpool nimewaangusha.”
Tukio hilo lilitokea kwenye uwanja wa Anfield wakati Ivanovic alipomzuia Suarez kwenye eneo la hatari la Chelsea.
Ivanovic alijaribu kumuonyesha mwamuzi Kevin Friend, sehemu aliyong’atwa na Suarez lakini mwamuzi hakuchukua hatua yoyote.
Bado haijajulikana hatua ambazo atachukuliwa, lakini mabosi wa FA wanalipitia tukio hilo.
Mashabiki wanalilia kuona Suarez anakutana na adhabu kali ikiwa ni pamoja na kufungiwa mechi nyingi, huku wengine wakitoa ushauri wa njia za kumzuia asirudie tena kufanya kitendo kama hicho.
Maoni ya Liverpool
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers alisema: “Baada ya kuangalia video ya tukio hilo, tabia yake haikubaliki na nimemwambia.”
Mkurugenzi Mkuu wa klabu, Ian Ayre alionya: “Tabia yake haiendani na mtu yoyote anayevaa jezi la Liverpool, tutalishughulikia swala hili ndani kwa ndani na tunasubiri maamuzi ya FA.”
Utata wa Suarez
Kabla ya Tukio hilo Suarez aliwahi kufungiwa mechi nane kwa kuonyesha matendo ya ubaguzi wa rangi dhidi ya beki wa kushoto wa Manchester United, Patrice Evra.
Kudaka mpira kwenye mstari wa goli kwenye mechi ya robo fainali dhidi ya Ghana, tabia ya kujiangusha na kutafuta penalti kwenye mechi za ligi kuu.
Desemba 2011, alifungiwa kutokana na kuwaonyesha ishara ya matusi mashabiki wa Fulham.
Oktoba 2013, alisherekea bao dhidi ya Everton kwa kujiangusha mbele ya David Moyes — ambaye aliwahi kusema kwamba wachezaji wanaojiangusha kama Suarez wanawakera mashabiki.
Maoni ya Wadau
Gwiji wa Liverpool, Graeme Souness alisema: “Sijawahi kuona kitu kama hiki kwenye mechi ya soka, hivi hutokea kwenye michezo ya kitoto, kila akiingia uwanjani lazima afanye kitu cha kijinga.”
Kiungo wa zamani wa Liverpool, Jamie Redknapp alisema: “Tofauti na matarajio ya wengi ameiangusha klabu.”
Tyson amkubali Suarez
Kitendo cha Luis Suarez kumng’ata Ivanovic amepata shabiki mmoja tu ambaye ni Mike Tyson.
Bingwa wa zamani wa uzito wa juu duniani, ambaye aliwahi kumng’ata sikio Evander Holyfield mwaka 1997, - alimfuata Suarez  kwenye mtandao wa Twitter dakika chache baada ya tukio hilo.
Tyson (46), alifungiwa kupigana baada ya tukio hilo na kutozwa faini ya pauni milioni 2.

No comments:

Post a Comment