Wednesday, January 9, 2013
SIMBA YAPAA KWA MAFUNGU KWENDA OMAN, WENGINE KUUNGANA NA TIMU JUMAPILI
TIMU ya Simba leo imeondoka nchini kuelekea nchini Oman kwa ajili ya mandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania Bara huku wachezaji wake watatu wakishindwa kuondoka kutokana na kukosa visa.
Wachezaji walikosa visa ni Paul Ngalema, Abdallah Juma na Keita, hivyo watawasubiri waondoke januari 13 mwaka huu na wenzao waliobaki na timu Zanzibar.
Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu Bara wameondoka saa tisa ikiwa na wachezaji nane na benchi la ufundi lenye watu wanne.
Waliondoka ni kocha mkuu Mfanransa Leiwing, Kocha msaidizi Basena, Daktari wa timu Cosmas Kapinga na Mtunza vifaa, Kessy.
Wachezaji waliondoka ni mlinda mlango Dhaira, Felex Sunzu, Kigi Makasy, Nassor Masoud "Cholo", Shamte Ally, Ramadhan Chombo na Salum Kinje.
Akizungumza baada ya timu kuondoka Katibu wa Simba, Mtawala alisema wanategemea kambi yao itakuwa na manufaa kwani hali ya hewa ya Oman inafanana na ya Dar es salaam japo timu imeondoka kwa makundi tofauti.
"Hali ya hewa ya Oman inafanana na Dar es salaam hivyo kuweka kambi huko itasaidia kuandaa timu kwa mzunguko wa pili", alisema Mtawala.
Pia alisema timu itakuwa wenyeji wa timu ya Fanja FC ya Oman na itakaa kwa wiki mbili.
Wachezaji walioko kwenye timu ya taifa wataungana na wenzao january 12 baada ya mchezo wao na Ethiopia utakaochezwa mjini Adidis ababa januari 11.
Wachezaji hao ni Juma Kaseja, Mrisho Ngassa,Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Shomari Kapombe na Amir Maftah.
Waliobaki Zanzibar kwenye kombe la Mapinduzi kwa ajili ya kumalizia mechi ya nusu fainali inayotarajiwa kuchezwa leo jioni na fainali kama timu itafuzu ni Ramadhan Singano, Jonas Mkude, Christopher Edward, Haruni, Seseme, Hassan na Miraji
Pia kiongozi wa msafara Said Pamba ataondoka na wachezaji waliobaki januari 13 mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment